• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC Malima atoa somo namna ya kuinua na kukuza Utalii kwa Wadau wa Sekta hiyo Kanda ya Ziwa

Posted on: September 6th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amewataka Wadau wa Utalii kuhakikisha wanatangaza vivutio vya Utalii vinavyopatikana katika  Mkoa huo ili kuwaleta watalii wengi zaidi katika vivutio mbalimbali siyo Serengeti na Ngorongoro peke yake.

Mhe.Malima ameyasema hayo leo Septemba 6, 2022 alipokutana na Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa Utalii alipowaita ili kuwapa mbinu, mikakati na namna bora ya kuboresha na kuinua Sekta hiyo.

"Lengo langu ni kutaka kuangalia kila mtu anauza nini, na kwa umoja wetu tuuze nini, ili mwisho wa siku tuunganishe nguvu ya pamoja katika kuutangaza utalii wa Mwanza,"alisema Mhe.Malima.

Mhe.Malima ameeleza kuwa Mwanza ni lango la kuingia Hifadhi ya Serengeti ambapo haichukui zaidi ya saa mbili kwa gari,pia alieleza ukaribu wa Mwanza na mbuga za Rumanyika, Kyerwa,Burigi- Chato,Kigosi na Rubondo.

Aidha, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane ACC. Eva Mallya amesema kunatakiwa kuwa na namna nzuri ya kutangaza Mwanza kwa kuwa na kipeperushi au Jarida ambalo litaonesha vivutio vyote vilivyopo Mwanza kwa pamoja.

"Tuunganishe  vivutio (packagies) hii itasaidia watalii wanaokuwepo Mwanza kuweza kutumia muda zaidi kuliko kuuza kivutio kimoja kimoja, kunakosesha thamani ya eneo,ni rahisi kukuza Saanane kwa kujumlisha na vivutio vingine mfano Bujora,"alisema Mallya.

Naye, Mkuu wa Idara ya Utalii Kanda ya Ziwa Dainess Kunzugala amesema Suala la utalii linategemea utayari wa miundombinu (airport) huduma za malazi pia linategemeana ushirikiano wa Serikali na Sekta binafsi, hivyo kuna umuhimu wa kuunda umoja wa wadau wa utalii (Association) kwa kanda ya ziwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Hifadhi ya Rubondo ACC.Moranda B.Moranda ameeleza kuwa wadau wote wa Utalii wanatakiwa kuangalia namna wanavyoweza kuwahifadhi wageni kwa upande wa vyakula, malazi na Gharama za Utalii na huduma mbalimbali kwani kwa kufanikisha hayo wanaweza kupokea watalii wengi zaidi kutoka sehemu mbalimbali.

"Tusimtazame mtalii kama tunavyojitazama sisi..... nahitaji kuoga naletewa maji kwenye ndoo...hii hatutafanikiwa, tutoke huko," alisisitiza Mhe.Malima.

"Katika hali ya kufanya Utalii wa Mwanza tufanye kama wanavyofanya wenzetu,tusifanye kama tulivyozoea wenyewe," ameongeza Mhe.Malima


Kwa upande wake, Kamanda Kikosi wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe ACC Yustin Njamas  amesema kuwa Viongozi wakielewa kuhusu swala hili la utalii watafanikiwa sana kwa sababu watapata ushirikiano mkubwa kutoka kwao na watakuwa  na mafanikio makubwa.

Aidha,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ibanda  ACC. Fredrick  Mofulu amesema tangu mtalii anapokelewa kuwe na uangalizi wa moja kwa moja lazima kuwe na utaratibu wa uangalizi na uwezo mkubwa wa kupokea wageni na kuwahudumia kwa ubora wa viwango pendekezwa kwa watalii.

Mmoja kati ya Wafanyabishara wakubwa Mwanza Bwana  Joel Charles Makanyaga  amesema kuwa Jiji kubwa la Mwanza linapitika kwa njia zote wadau wa Sekta ya Utalii wanatakiwa wakae kwa pamoja ili waje na mpango wa pamoja ili kukuza uchumi na utalii wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.