• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC Malima awapa somo wachezaji wa Pamba namna ya kupanda Ligi kuu msimu ujao

Posted on: November 2nd, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amewataka wachezaji wa timu ya soka ya Pamba inayoshiriki ligi ya Championship kucheza kwa malengo na hatimaye kupanda ligi kuu msimu ujao.

Akizungumza leo na wachezaji na uongozi wa klabu hiyo kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana Mkuu huyo wa Mkoa amesema mchezaji anayecheza bila ya malengo huyo hafai na aondolewe kwenye timu kwenye dirisha dogo.

"Kwangu mimi nina mambo mawili ambayo sikubaliani nayo kucheza bila malengo na migogoro mkinionesha hali hiyo najiweka kando nanyi", amesisitiza Mhe.Malima

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye ameinua soka kwenye Mikoa aliyofanya kazi ya Mara na Tanga amesema hivi sasa anaendelea kutunisha mfuko wa kuendeleza soka Mkoani Mwanza na wadau wamekuwa na imani na mwendo wa timu ya Pamba hivyo amewataka wasimuangushe kwa kufanya mambo yasiyo na tija.

Aidha, Mhe. Malima kwenye Mkutano huo na wachezaji wa Pamba amewakabidhi Shilingi Milioni moja kama motisha baada ya kufanya vizuri michezo yao miwili ya ligi Daraja la kwanza kwa kuilaza Pan African bao 1-0 kabla ya kuibugiza Trans Camp mabao 2-0.

"Jiwekeeni utaratibu wa kucheza soka la kisasa na kutanguliza nidhamu hii ndiyo siri ya nyota wengii wa soka Duniani walivyofanya pia wekeni luninga kubwa kwenye hostel yenu mtakayotumia kuona mchezo mlioshiriki na kubaini makosa au sehemu mliofanya vizuri kuongeza zaidi maarifa, kwa kufanya hivyo mtawavutia wafadhili kutokana na kuwa na timu inayofanya vizuri wakati wote," Amesema Mkuu wa Mkoa.

Awali akimkaribisha Mhe. Malima, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano

 wa klabu hiyo Aleem Alibhai amemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa moyo wa kupigania timu hiyo na kusisitiza motisha wanayopata kutoka kwa wadau inawaongezea ari ya kufikia malengo yao ya kucheza ligi kuu.

Timu ya soka ya Pamba katika msimamo wa ligi Daraja la kwanza inashika nafasi ya 6 ikiwa na mtaji wa pointi 15 na mwishoni mwa wiki hii watashuka dimbani Nyamagana kumenyana na timu ya Ndanda kutoka Mtwara.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. July 29, 2022
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2022 July 03, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI ICAP October 21, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC Malima awataka Madiwani kusimamia na kuendeleza vyema rasilimali za Bonde la Ziwa Victoria

    March 31, 2023
  • RC Malima awahimiza Wana Mwanza kufurika Dimbani Nyamagana Jumamosi hii kuwashangilia wana TP LINDANDA Pamba FC dhidi ya Kitayose

    March 30, 2023
  • Makinda awataka wasomi na wananchi kuyatumia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kujiinua kiuchumi

    March 29, 2023
  • RC Malima ahimiza kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia

    March 27, 2023
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 33180, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.