• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC Mongella atekeleza kwa Vitendo agizo la Mhe.Rais

Posted on: August 18th, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ametekeleza agizo lililotolewa na Mhe. Rais Dkt.John Pombe  Magufuli juu ya kuhakikisha anasimamia na kuyafanyia maamuzi  malalamiko ya wafanyabiashara wadogo Maarufu Machinga wilayani Sengerema.

Hii ni kufuatia maagizo ya Mhe.Rais Dkt.John Magufuli baada ya kupita Wilaya ya Sengerema akielekea Wilaya ya Chato kwa ajili ya mapumuziko na kusimama kwa ajili ya kuwasalimia, ndipo walipotoa malalamiko kuwa mnamo tarehe 10.8.2018  ilifanyika operation ya kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo, hiyo ilipelekea wafanyabiashara  wa nanasi 11 wanaofanya biashara ya kuuza nanasi kandokando ya barabara  kuchukuliwa na Halmashauri katika oparesheni hiyo.

Mhe.Mkuu wa Mkoa amemtaka mkurugenzi kulifanyia marekebisho soko lililipo karibu na eneo wanalouzia nanasi kwa sasa  kwa kujenga mabanda ya nguzo za mabomba yatakayoezekwa  kwa mabati ili kuwatengenezea kivuli baada ya hapo wafanyabiashara hao washirikishwe katika kupanga na kuhamia katika eneo hilo.

"Ifikapo jumatatu tarehe 20/08/2018 wale  watu 11 waliochukuliwa biashara zao za nanasi waitwe  na  wafidiwe fedha kwa nanasi zao kuchukuliwa  kwa jinsi watakavyokuwa wamekubaliana na ifikapo jumatano tarehe 22/08/2018 wawe wamelipwa fidia yao,"alisema Mongella.


Aidha Mhe Mongella  amemuagiza mkurugenzi huyo kuwa maafisa maendeleo ya jamii watumike kwenda kwenye jamii kuwaelewesha na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa masuala  mbalimbali yenye tija kwa kjamii na  sio watu  wa mapato ambao kazi yao ni kukusanya mapato.

Naye Jacob Mlinga mmoja kati ya wananachi walioathirika na kuchukuliwa nanasi zao na watendaji wa Halmashauri ya Sengerema amemwambia Mhe. Mkuu wa Mkoa kuwa alichukuliwa nanasi 700 yaliyokuwa kwenye matoroli mawili, ambapo baada ya  kumsikiliza aliwaelekeza yeye na wenzake kwenda ofisini kwa mkurugenzi ambapo tatizo lao litashughulikiwa.


Kwa upande wake mfanyabiashara mwingine Elina Taibu anayejishughukisha na biashara ya umachinga amemshukuru Mhe.Rais John Pombe Magufuri kwa kuwajali wanyonge na ameomba aendelee kuwatetea na kushughulikia matatizo ya watu wa chini.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Magesa Mafuru Boniface amewataka wafanyabishara waendelee kutoa ushirikiano kuhamia katika eneo lililotengwa la kisima cha chumvi, pia  amempongeza Mhe. Rais kwa kusikiliza kero za wananchi wa Sengerema na kuahidi kutekeleza maagizo yote aliyoagizwa kuyatekeleza katika kushughulikia tatizo la wafanyabiashara  

hao.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.