• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA AAGIZA FIDIA MILIONI 163 ILIPWE HARAKA KISOKO SEKONDARI

Posted on: February 12th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwalipa wananchi fidia ya shilingi milioni 163 zilizobaki ili kupisha ujenzi wa mabweni katika Shule mpya ya Sekondari Kisoko.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shule hiyo iliyopo Kata ya Luchelele, RC Mtanda amesema tayari shilingi milioni 187 zimelipwa, huku kiasi kilichobaki kikihusu wananchi 11. Amesisitiza malipo hayo yakamilike haraka ili maandalizi ya ujenzi wa mabweni yaanze bila kuchelewa.

Aidha, ameipongeza Halmashauri kwa kusimamia vyema mradi huo hadi kukamilika kwake, akiwataka viongozi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwa kuwa kazi ndiyo kipimo cha uongozi bora.

RC Mtanda pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi milioni 584 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo. Amesema miundombinu ipo tayari na walimu wameajiriwa, hivyo wazazi wahakikishe wanafunzi wote waliochaguliwa Kidato cha Kwanza wanaripoti shuleni.

Sambamba na hilo, amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha maabara angalau moja inakamilishwa ndani ya mwaka huu ili kuanza mpango wa maabara nyingine mwakani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisoko Aloyce Bihege amesema shule imejengwa kupitia mpango wa kuboresha elimu ya sekondari (SEQUIP) kwa mwaka wa fedha 2024/2025, na ilipokea shilingi 584,280,029 tarehe 08 Oktoba 2024. Masomo yalianza rasmi tarehe 08 Julai 2025 na wanafunzi 147 (wavulana 67 na wasichana 80) kutoka Luchelele Sekondari.

Hadi tarehe 12 Februari 2026, shule ina jumla ya wanafunzi 290, wakiwemo 143 wa Kidato cha Kwanza 2026 (wavulana 71 na wasichana 72) kati ya 215 waliopangwa kujiunga mwaka huu. Ameongeza.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI IDARA YA MAAFA OWM AFUNGA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA DHARULA MWANZA

    February 20, 2026
  • KAYA 19,344 KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE MWANZA AWAMU YA KWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AMPOKEA WAZIRI DEUS SANGU MWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AWATAKA WASIMBE NA WABANZA KUUNGANA KUKATA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 20, 2026
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.