• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA AAGIZA KUFANYIKA KWA TATHMINI MIUNDOMBINU YA SHULE

Posted on: February 10th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amezielekeza Halmashauri zote za Mkoa huo kufanya tathmini ya kina ya changamoto na upungufu wa miundombinu katika Shule za Msingi na Sekondari ili kubaini mahitaji halisi na kuyaainisha mapema kabla ya kupatiwa fedha za utekelezaji.

RC Mtanda amesema si busara kwa changamoto za shule kusubiri kuibuliwa kwanza kupitia mitandao ya kijamii ndipo hatua zichukuliwe, badala yake tathmini ifanyike mapema ili kuzuia aibu na usumbufu kwa wanafunzi.

Ameyasema hayo alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari Masemele iliyopo Wilayani Ilemela ambapo amesema amekuwa akipokea ujumbe kutoka kwa wazazi wakilalamikia uhaba wa madawati katika baadhi ya shule za Wilaya hiyo.

“Ni aibu kubwa kuona wanafunzi wamekaa chini, halafu picha zinasambazwa mitandaoni ndipo tuanze kukimbizana kutafuta suluhu. Tusifikie huko,” amesema RC Mtanda.

Ameelekeza tathmini ifanyike kwa shule zote za msingi na sekondari ili kubaini maeneo yenye upungufu wa madawati, vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na miundombinu mingine muhimu, ili fedha zitakapopatikana zielekezwe moja kwa moja kwenye mahitaji hayo.

Aidha, amewataka watumishi wa sekta ya elimu kuelewa mazingira yao na kuweka vipaumbele kulingana na uhitaji mkubwa uliopo katika maeneo yao.

Katika hatua nyingine, RC Mtanda ametoa maagizo ya kukamilika kwa ujenzi wa maabara hiyo ndani ya wiki mbili, pamoja na kukamilisha uwekaji wa nishati ya umeme katika chumba kimoja cha maabara na kufunga tenki la maji ili kuwezesha matumizi bora ya miundombinu hiyo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MTANDA AWATAKA WASIMBE NA WABANZA KUUNGANA KUKATA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AZINDUA SHULE YA SEKONDARI BUMYENGEJA KWIMBA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AZINDUA NYUMBA YA WATUMISHI KITUO CHA AFYA BUDUSHI, ATOA WITO KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 20, 2026
  • RAS MWANZA AHIMIZA MATUMIZI YA FURSA ZA MICHEZO

    February 19, 2026
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.