• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA ALIPONGEZA JIJI LA MWANZA KWA HATUA YA KUJIKWAMUA NA UPUNGUFU WA MADAWATI

Posted on: February 12th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa juhudi zake za kupunguza upungufu wa madawati katika shule za elimu ya awali na msingi, akisema hatua hiyo ni kielelezo cha uwajibikaji na dhamira ya dhati ya kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.

RC Mtanda ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi jumla ya madawati 2,939 kwa shule 13 za elimu ya awali na msingi zilizopo ndani ya Jiji la Mwanza. Madawati hayo yametengenezwa kwa thamani ya Shilingi 440,800,000 katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo.

Amesema kwa sasa Mkoa wa Mwanza una upungufu wa madawati 61,808, huku Jiji la Mwanza likiwa miongoni mwa halmashauri zenye uhaba mkubwa zaidi. Hata hivyo, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji hilo kwa kuanza mchakato madhubuti wa kumaliza changamoto hiyo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa, utekelezaji wa mradi huo utaondoa upungufu wa karibu madawati 4,000 na kubakiza takribani 2,000 pekee, ambayo ameahidi yataondolewa mapema mwaka huu.

“Nimefurahi kusikia kuwa Mkurugenzi ameahidi kumaliza kabisa uhaba wa madawati katika halmashauri yake. Nawataka Wakurugenzi wengine waige mfano huu,” amesisitiza.

Aidha, RC Mtanda aliziagiza halmashauri zote zenye upungufu mkubwa wa madawati ikiwemo Jiji la Mwanza, Kwimba, Magu na Sengerema kuanzisha karakana za utengenezaji wa madawati ili kupunguza gharama na kuongeza kasi ya uzalishaji. Alionya kuwa ndani ya miezi mitatu Ofisi yake itaanza kufanya ziara za ukaguzi kufuatilia uzalishaji huo, akisisitiza kuwa ifikapo mwisho wa mwaka huu changamoto ya madawati iwe historia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wakili Kiomoni Kibamba, amesema wamejipanga kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini darasani. Ameeleza kuwa kipaumbele kimetolewa kwa shule zenye mahitaji makubwa na kwamba ifikapo mwezi Juni mwaka huu, madarasa yote yaliyopo yatakuwa na wastani wa madawati 30 kila moja.


Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI IDARA YA MAAFA OWM AFUNGA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA DHARULA MWANZA

    February 20, 2026
  • KAYA 19,344 KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE MWANZA AWAMU YA KWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AMPOKEA WAZIRI DEUS SANGU MWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AWATAKA WASIMBE NA WABANZA KUUNGANA KUKATA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 20, 2026
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.