• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA KAMPASI YA TAASISI YA UHASIBU

Posted on: July 10th, 2024

RC MTANDA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA KAMPASI YA TAASISI YA UHASIBU


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameridhishwa na ubora, kiwango na kasi ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kanda ya Ziwa, unaotekelezwa katika Kata ya Nyangomango Wilayani Misungwi.

Akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo leo Julai 10, 2024, Mhe. Mtanda amesema mradi huo umemvutia sana na unapendeza hata kwa macho ambapo pia amesema uwepo wa Taasisi hiyo  kumechagiza kuzaliwa kwa ajira mbalimbali kwa wakazi wa Nyangomango, Misungwi na Mwanza kiujumla.

"Mradi ni mzuri sana lakini lazima tuwe na mikakati ya kuboresha huduma za miundombinu, tunataka kuwepo na kituo hapa cha kusimama na kupakia abiria ili hata hawa bodaboda, bajaji na usafiri mwingine waweze kupata ajira".Mtanda

Sisi tunahitaji kuona kituo kimekamilika kabla ya wanafunzi hawajafika hapa, hatuhitaji maneno maneno, tunahitaji utekelezaji wa maelekezo, kwa hiyo hilo ninaamini mtalitekeleza kama mlivyosema mtaanza na kituo cha muda. Amesema Mkuu wa Mkoa.

Aidha Mhe.Mtanda ametoa maagizo kwa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa ardhi (LATRA) na wakala wa barabara za Tanzania (TANROADS) kuhakikisha wanatenga bajeti ya utengenezaji wa miundombinu ya kudumu ya barabara za kuingia na kutoka chuoni hapo ili mwakani barabara hizo zianze kutengenezwa.

Kadhalika Mkuu wa Mkoa amemuhakikishia Mkuu wa Chuo na wananchi wa Usagara na Misungwi kuwa Serikali ya Rais Samia imejipanga kwenye sekta ya maji kwa kuamua kuwekeza fedha zaidi ya Tshs. Bilioni 70 ambapo tayari chanzo cha maji kimeshajengwa na baada ya hapo kitakachofuata ni kusambaza huduma ya maji kwa wananchi.

"Sasa hivi tumepata bilioni 49,  mkandarasi anarudi kazini kwa ajili ya kupanua miundombinu ya usambazaji maji na wananchi wa usagara wote watapata maji na hiki chuo pia kitapata maji",amesisitiza mkuu huyo wa mkoa

Akitoa Taarifa ya ujenzi wa kampasi hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Kampasi ya Mwanza Dkt. Honest Kimario, amesema  ilianzishwa mwaka 2021 katika Kataya Nyakato Wilayani Ilemela lengo ikiwa ni kusogeza huduma kwa wakazi wa kanda ya ziwa.

Lakini kutokana na kuongezeka kwa uhitaji wa huduma za Taasisi kwa wananchi ambapo hapo awali walikua wamepanga wameamua kunununua kiwanja hicho ndani ya Wilaya ya Misungwi chenye ukubwa wa mita za mraba 148,000 sawa na hekari 61 kwa ajili ha ujenzi wa miundombinu ya kudumu.

"Mwaka 2022 Taasisi ilipata fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 7.8 kutoka Wizara ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kudumu na taasisi ilianza mradi 22.01.2022 na mradi unatarajiwa kukamilika 21.07.2024." Amesema Dkt. Kimario.

Mradi huo umeshakamilika kwa 98.5, aidha  unajumlisha madarasa yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1100 kwa wakati mmoja ndani yake kutakua na maabara na maktaba ya kisasa ambapo jumla kuu ya wanafunzi wanaoweza kuhudumiwa kwa wakati mmoja ni 4650 kwa siku.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MWANZA, SIMIYU ZANG'ARA UTAMILIFU DARASA LA SABA KANDA YA ZIWA

    May 30, 2025
  • RAS MWANZA AZINDUA RASMI MRADI WA KUPAMBANA NA UGONJWA WA SELI MUNDU

    May 30, 2025
  • WAANDISHI WA HABARI MWANZA WAPIGWA MSASA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA WATOTO WA MITAANI

    May 29, 2025
  • RAS MWANZA AWATAKA VIONGOZI WA UMMA KUDUMISHA NIDHAMU NA UFANISI KAZINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.