RC MTANDA ASHIRIKI MAZISHI YA MZEE SILVIN MONGELLA
Leo Juni 07, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameshiriki mazishi ya Mzee Silvin Ibengwe Mongella, Baba Mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara na Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (2015-2021) Mhe. John Mongella.
Ibada ya mazishi hayo imefanyika katika Mtaa wa Kabusungu Wilayani Ilemela na kuongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Tiafa Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mawaziri wa Wizara mbalimbali, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Taasisi, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Wanananchi mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.