• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA AWATAKA WATAKWIMU KUTOA TAKWIMU SAHIHI KUCHAGIZA MAENDELEO

Posted on: November 18th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka Wataalamu wa Takwimu nchini kuchakata kwa weledi na kutoa takwimu na taarifa sahihi kwa jamii ili kuwapa mwelekeo wa shughuli za kufanya kwa wakati fulani ili kupata maendeleo.

Mhe. Mtanda ametoa wito huo mapema leo tarehe 18 Novemba, 2025 wakati akizungumza na wataalamu wa Takwimu kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa waliokutana kwenye maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.

Amesema wananchi wanapanga maisha yao kiuchumi na kijamii kwa kutegemea taarifa sahihi kutoka serikalini mathalani kuhusu bei za bidhaa au hali ya upatikanaji wa pembejeo hivyo wanawategemea kuwapatia taarifa sahihi za namna gani waenende.

“Mipango, taarifa na takwimu sahihi ndizo zinazotuwezesha kufanya makadirio ya maisha ya baadaye hivyo basi ninyi ndio wataalamu mnaotegemewa kufanya utafiti na kutumia ubunifu wa kuchakata na kutoa taarifa sahihi kwao ili kuwapa mwelekeo hivyo siku zote lazima muzingatie hilo.”

Ameongeza kuwa Dira ya taifa ya maendeleo kwa 2025/2050 inawategemea wataalamu hao katika kuweka misingi na mikakati ya uwekezaji na uwajibikaji katika kwenye kila sekta hivyo takwimu zina faida kubwa kwenye kupanga mifumo ya maamuzi sahihi ya maendeleo.

“Pamoja na kwamba takwimu zinasaidia kuweka misingi sahihi katika kupanga maendeleo zinasaidia pia kukuza utafiti na uvumbuzi, kuimarisha uchumi na uwekezaji, kuweka taswira ya ukweli, kuboresha huduma za jamii pamoja na kuboresha ufanisi na kupunguza hasara” Amesisitiza RC Mtanda.

Aidha, amewapongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kutekeleza kwa ufanisi jukumu kubwa la Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika kwa mafanikio mwaka 2022 nchini na ametoa wito kwa wananchi kusoma taarifa za tume hizo katika tovuti na mbao za matangazo ili kupata taarifa sahihi za mambo mbalimbali.

Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika ambayo yameanza rasmi mwaka 1990 baada ya mkutano wa Mawaziri wa Uchumi na Mipango wa nchi za Afrika (Addis Ababa) kwa mwaka 2025 yanachagizwa na kaulimbiu ya ‘Kuongeza Ubunifu katika Matumizi ya Takwinu na Taarifa ili kujenga Jamii Jumuishi

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RAS BALANDYA AMEWATAKA WAHITIMU IFM KUWA MABALOZI WAZURI WA CHUO CHAO

    December 06, 2025
  • RC MTANDA AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZINAZOPATIKANA

    December 06, 2025
  • SERIKALI YATENGA FEDHA KUKAMILISHA MIRADI YA MAENDELEO MWANZA - DKT. NCHEMBA

    December 05, 2025
  • DKT. NCHEMBA ATOA POLE KWA WANANCHI WALIOHARIBIWA MALI KUTOKANA NA VURUGU MKOANI MWANZA

    December 05, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.