• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA AZINDUA NYUMBA YA WATUMISHI KITUO CHA AFYA BUDUSHI, ATOA WITO KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Posted on: February 20th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amezindua mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi (2 in 1) katika Kituo cha Afya Budushi, Wilaya ya Kwimba Mradi uliotekelezwa kwa ushirikiano kati ya TASAF Awamu ya Tatu kupitia mpango wa TPRP IV na wananchi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Sumve.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Mhe. Mtanda ameipongeza Serikali kwa juhudi za kuimarisha sekta ya afya mkoani Mwanza. Amesema ujenzi wa nyumba za watumishi utasaidia kuboresha mazingira ya kazi kwa wahudumu wa afya na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.

Aidha, amewahamasisha wananchi wa Kwimba na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla kuchangamkia mpango wa Bima ya Afya kwa Wote unaotarajiwa kuzinduliwa kimkoa Februari 20, 2026 katika Wilaya ya Misungwi. Amesema kila kaya itachangia shilingi 150,000 na kunufaika na huduma 378 za afya.

Akisoma taarifa ya mradi, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Budushi, Dkt. Paulo Kanga amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ilipokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za watumishi (two in one) katika kituo hicho. Mradi huo uliibuliwa na wananchi wa Kijiji cha Sumve mwaka 2023.

Utekelezaji wa mradi ulianza Aprili 30, 2025 ukisimamiwa na Halmashauri kwa kushirikiana na Kamati ya Usimamizi wa Mradi (CMC) ya kijiji. Mradi huo ulifadhiliwa na TASAF kupitia mpango wa kupunguza umaskini awamu ya nne (TPRP IV).

Jumla ya gharama za mradi zilikuwa Sh. 205,521,170.58, ambapo TASAF-OPEC ilitoa Sh. 184,821,428.58 na jamii ilichangia Sh. 20,699,742.00 kupitia vifaa vya ujenzi vinavyopatikana eneo husika na nguvu kazi ikiwemo usafirishaji wa maji, mchanga, kokoto, mawe na umwagiliaji maji wakati wa ujenzi.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI IDARA YA MAAFA OWM AFUNGA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA DHARULA MWANZA

    February 20, 2026
  • KAYA 19,344 KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE MWANZA AWAMU YA KWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AMPOKEA WAZIRI DEUS SANGU MWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AWATAKA WASIMBE NA WABANZA KUUNGANA KUKATA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 20, 2026
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.