• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA AZINDUA RASMI BODI YA USHAURI HOSPITALI YA SEKOU TOURE,AHIMIZA MABORESHO

Posted on: December 14th, 2024

RC MTANDA AZINDUA RASMI BODI YA USHAURI  HOSPITALI YA SEKOU TOURE,AHIMIZA MABORESHO


Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe: Christopher Ngubiagai amezindua rasmi Bodi ya ushauri ya Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Seko Toure na kutoa rai kwa wajumbe wa bodi  hiyo wazingatie mikakati na maamuzi yanayolenga kuboresha huduma, kuwakilisha maslahi ya wananchi Kwa uwazi na uadilifu na kuhakikisha rasilimali za Hospitali zinatumika Kwa njia bora.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza comrade Ngubiagai amebainisha ni wajibu wa Bodi hiyo ya Afya  kuhamasisha uwekezaji katika mifumo ya kidigitali, kuanzisha programu ya mafunzo Kwa watoa huduma,kukuza ushirikiano na wadau wa sekta ya afya na Kuboresha ufanisi wa kuongeza mapato ya Hospitali.

"Tumeona juhudi za Serikali namna inavyoboresha sekta ya afya,miradi mingi imeletwa mkoani Mwanza na hospitali hii sasa inatoa huduma nyingi za kibingwa,tunapaswa kuunga mkono juhudi hizi kwa kuleta ubunifu zaidi wenye tija,"amesisitiza mkuu huyo wa wilaya wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa bodi hiyo ya ushauri.

Ameongeza kuwa kupitia Bodi ya ushauri yenye wataalam wa sekta ya afya ni wajibu wao kuhakikisha wanaleta mageuzi chanya kwa kuimarisha usimamizi wa rasilimali, ufuatiliaji, uwajibikaji wa watendaji na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Bw. Alhaji Sibtain Meghjee amesema uzinduzi wa Bodi hiyo utakuwa na kielelezo tosha cha kuimarisha na kuboresha huduma na wananchi watapata huduma bora na kwa wakati

Katika hatua nyingine Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Dkt.Bahati Msaki amemshukuru mgeni rasmi  kwa kuzindua Bodi ya Ushauri ya Hospitali na kuahidi  kutoa ushirikiano kati ya bodi hiyo na watumishi wa Hospitali ya Sekoutoure ili kuendelea kuboresha huduma za afya

Sanjali na uzinduzi huo pia Mkuu huyo wa wilaya na wajumbe wa bodi walifanya ziara na kukagua huduma mbalimbali zitolewazo Hospitalini hapo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.