• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC Mwanza aendelea kuwakaribisha Wananchi wa Mwanza Jumamosi hii katika muendelezo wa utambulisho wa Filamu ya ROYAL TOUR

Posted on: June 16th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Injinia Robert Gabriel ameendelea kuwaalika  wananchi wa Mkoa huo kushiriki Utambulisho rasmi wa Filamu ya Royal Tour kwenye viwanja vya Rock City Mall itakayotanguliwa na burudani za ngoma na wasanii Jumamosi ya Juni 18, 2022 kuanzia saa 9 alasiri.


Ametoa salamu hizo leo kwa niaba yake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe Veronica Kessy alhamisi ya Juni 16, 2022 akiwa kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti alipowaongoza wananchi zaidi ya 150  waliofika kwenye hifadhi hiyo kuangalia wanyama na vivutio vya Utalii.


"Baada ya Uzinduzi wa Filamu hii nchini Marekani na baadae hapa nchini, Mhe Waziri Mkuu ametoa maagizo ya kuzindua filamu hii mikoani hivyo katika kuelekea kwenye kuizindua rasmi filamu hiyo tumeanza kwa kufanya utalii wa ndani hapa Serengeti na kesho tutatembelea vivutio ndani ya Mkoa wa Mwanza na jumamosi sasa itakua ndio siku rasmi ya Utambulisho." Mhe Kessy.

"Nawakaribisha wananchi wote wa Mwanza kwenye viwanja vya Rock City Mall siku ya Jumamosi kwa ajili ya kutazama filamu ya Royal Tour tuone namna gani mama ameitangaza nchi yetu lakini vilevile Utamaduni wa watu wa Mwanza utaoneshwa pale," amebainisha.

"Tunampongeza Mhe Rais kwa kufanya filamu ya ROYAL TOUR kwani imesaidia kuongeza watalii nchini na kwa wananchi inawapa fursa moja kwa moja kunufaika kupitia kutoa huduma kama za chakula na imesaidia kuwaonesha watanzania kuwa Hifadhi zetu ni za kujivunia." Mhe. Jonas Lufungulo Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza.


"Sisi kama Serengeti tumefurahi sana kupokea ugeni huu mkubwa na haya ni matunda ya Filamu aliyoifanya Mhe Rais mwenyewe kwenyewe Hifadhi mbalimbali nchini ikIwemo hii na kwakweli katika kipindi cha janga la Uviko wageni na pato la serikali lilishuka kupitia Utalii lakini hivi sasa wameongezeka kwa wingi." Regius Komba Mhifadhi mwandamizi

"Hali ya utalii wa ndani baada ya filamu ya Royal Tour ni kwamba imekua zaidi kama hivi leo tumepokea zaidi ya watalii 150 kwenye ukanda huu wa magharibi mwa Serengeti, na hifadhi yetu imeongoza miaka mitatu mfululizo kuwa Hifadhi Bora na Mwaka huu inawania tena nafasi hiyo hivyo nawaomba watanzania wapige kura kupitia tovuti ya Best African Travel Awards." Ameelezea Bwana Komba.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.