• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

SAUT wamkumbuka Hayati Mkapa kwa kutoa Mikopo Wanafunzi Vyuo binafsi.

Posted on: November 12th, 2022

*SAUT  wamkumbuka Hayati  Mkapa kwa  kutoa Mikopo Wanafunzi Vyuo Binafsi*



Makamu  Mkuu wa Chuo Kikuu  cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Profesa Costa Ricky Mahalu, amesema Hayati Benjamin William  Mkapa  atakumbukwa kwa kushawishi sekta binafsi kuwekeza nchini  hasa katika maswala ya elimu ya juu hali iliyosaidia kuongeza kiwango  kikubwa cha wahitimu wa vyuo vikuu nchini.

Akizungumza Chuoni hapo  leo Novemba 12, 2022 kwenye uzinduzi wa Kigoda cha  Utafiti cha Benjamin Mkapa, Profesa Mahalu amesema  Mkapa aligusa maisha ya watanzania wengi kwani akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  serikali ilianza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu  wenye sifa waliokuwa wakisoma  vyuo vikuu  binafsi mwaka 1995.

"Hayati Mkapa aligusa sana sekta binafsi hasa katika elimu leo hatuwezi kufurahia tukiwa na vijana wengi waliohitimu vyuo vikuu bila kumtaja, mtakumbuka  kabla ya mwaka 2005  Serikali ilikuwa ikitoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya serikali peke yao, hivyo vijana wengi wenye sifa ya kusoma vyuo vikuu walikosa fursa kutokana na wazazi au walezi kushindwa kumudu gharama.

"Mwaka 2001 alipokuja hapa chuoni SAUT  kwenye mahafali ya kwanza akiwa mgeni rasmi wakati huo alikuwa  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania aliahidi wanafunzi wa vyuo vikuu binafsi wenye sifa wataanza  kupata mikopo kabla hajatoka madarakani, wakati huo  SAUT ilikuwa na wanafunzi chini ya 400 leo tunawanafunzi zaidi ya 16,000, mafanikio hayo yametokana na mikopo inayotolewa na Serikali,"amesema Balozi Profesa Mahalu.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Uganda, Profesa John Mugisha, amesema Hayati Mhe. Mkapa alikuwa ni kiongozi anayesikiliza watu wengine wa kada mbalimbali hata kama wanatofautiana itikadi pia alikuwa tayari kufanya kazi na  watu wanaotoka  mataifa ya nje.

Mkuu wa Idara ya Falsafa kutoka Chuo cha SAUT, Padri Dkt.Innocent Sanga, amemuelezea Hayati Mhe.Mkapa  kwamba alikuwa  mchambuzi na mkosoaji,  hakupenda ubaguzi alikuwa anapenda kusali,alikuwa anasikiliza ushauri na kufanya maamuzi makini bila kuyumba.

"Alikubali kushindwa kwa hoja alikuwa na fikra yakinifu na bunifu, washauri wabaya enzi za uongozi wake hawakuwa na nafasi kwake,"amesema Padri Dkt. Sanga.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mchumi aliyebobea  amesema, Hayati Mhe.Mkapa ameacha alama ambayo inagusa  mioyo, macho na masikio ya vizazi vya sasa na vijavyo kwani alishika madaraka kukiwa na mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kisiasa lakini aliyatengenezea misingi na kuyasimamia

kwani aliamini katika utekelezaji wa uchumi wa  ubia.

"Nipende kuwahakikishieni kuwa yapo mambo mengi kwenye Serikali ya awamu ya sita ya Mhe.Samia Suluhu Hassan ambayo ni mwendelezo wa yale aliyoyayaanzisha  Mhe. Hayati Mkapa  ikiwemo bima ya afya ambayo sasa Serikali iko katika mchakato wa kuhakikisha kila Mtanzania anufaika nayo.


Akimzungumzia Hayati Mhe.Mkapa, Balozi  Profesa Ombeni Sefue, ambaye alikuwa mzungumzaji Mkuu kwenye uzinduzi huo amesema alikuwa akiheshimu haki ya kuishi     na hilo alilithibitisha  kwa kutotia saini ya watu waliohukumiwa kunyongwa ili wanyongwe.

Pia alitumia muda wake mwingi kusoma vitabu na majarida badala ya kukaa kijiweni na kuongea mambo yasiyo ya faida kwa jamii maana aliamini

 kwamba vitabu ni muhimu katika kurutubisha akili nafsi, moyo na roho ya mwanadamu.

Balozi Profesa Sefue ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Viongozi Dar  Es  Salaam ameendelea kumuelezea Hayati Mhe. Mkapa kwamba alikuwa ni mwaminifu ambapo alipenda kusema ukweli na uwazi, mara kwa mara alisema bora achukiwe  kwa kusema ukweli kuliko kupendwa kwa kudanganya.

Naibu Mkuu wa Skuli ya Sheria - Taaluma Zanzibar, Wakili  Msemo Mavare amesema  tasnia ya sheria itamkumbuka Hayati Mhe. Mkapa kwa mchango wake katika utawala wa sheria kwani ndiye Rais mstaafu  pekee Afrika aliyekwenda mahakamani kutoa ushahidi  kumtetea Profesa Costa Ricky Mahalu wakati anashtakiwa, alikuwa tayari kuhojiwa ili haki itendeke.


Mwisho

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.