• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

SERIKALI IMEKUJA NA NJIA ZA KUDHIBITI UBORA NA USALAMA WA CHAKULA NA VIPODOZI

Posted on: June 9th, 2023

*SERIKALI IMEKUJA NA NJIA  ZA KUDHIBITI UBORA NA USALAMA WA CHAKULA NA VIPODOZI*


 *TBS yasaini  mkataba wa mashirikiano katika utekelezaji wa kanuni ya ushirikiano na Halmashauri za Mwanza*


 *Serikali yadhamilia kupanua wigo wa kudhibiti ubora na usalama wa chakula na vipodozi*


 *TBS Yagawa Vishikwambi kila Halmashauri kurahisisha utekelezaji wa shughuli za ukaguzi*



Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana amesema Serikali imekuja na njia za kuhakikisha shughuli za kudhibiti ubora na usalama wa chakula na  vipodozi zinafanyika kwa uharaka na kwa ufanisi ili kuhakikisha bidhaa zilizopo  sokoni zipo kwenye viwango vinyofaa.

Amesema hayo leo tarehe 09 Juni, 2023 wakati wa *uwekaji wa saini katika mkataba wa mashirikiano katika utekelezaji wa kanuni ya ushirikiano ya mwaka 2021 baina ya  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Jiji za Mkoa wa Mwanza.*

"Azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa  inakuwa na mtandao mkubwa unaoshughulikia shughuli za *udhibiti wa ubora na usalama wa chakula na vipodozi* kwa kulitekeleza hili serikali imeamua kuwatumia  wakaguzi walio chini ya Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika shughuli za udhibiti wa bidhaa husika ili kulinda afya za watumiaji katika maeneo yao," amesema Ndg. Elikana.

Zoezi la uwekaji wa saini katika mkataba huo limeambatana na *ugawaji wa vishkiwambi ambavyo vitawasaidia  katika utendaji kazi* kwa waratibu wa TBS waliopo katika Halmashauri ambapo Ndg. Balandya amewataka  kuhakikisha vitendea kazi hivyo vinafanya kazi kwenye majukumu husika.

" Napenda ieleweke kuwa kitendea kazi hiki sio mali binafsi ya mtumishi atakayekabidhiwa bali ni mali ya Halamashauri  na kwamba Mkurugenzi wa Halmashauri anao wajibu wa kuhakikisha kitendea kazi kinatumika kwa majukumu  kusudiwa na endapo  mtumishi aliyekabidhiwa  akihamishiwa ama kubadilishiwa majukumu basi aliyeteuliwa badala yake akabidhiwe ili kuendeleza majukumu ya udhibiti," ameongeza Ndg.Balandya.


Naye, Meneja wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Happy Kanyeka  amesema baada ya kukasimisha majukumu hayo kwenye ngazi za Halmashauri italeta wepesi katika kuwafikia wananchi wa ngazi ya chini na kuwapatia  huduma  kwa uharaka.

"Baada ya kukasimisha majukumu kwenye halamashauri  huduma zitakwenda kufika hadi kwenye ngazi za kata  kwa kuwa watumishi  wa TBS tulikuwa hatuwezi kufika katika halamashauri zote lakini tukaona madalaka kukasimishwa kwenye ngazi  za Halmashauri huduma zitapatikana kwa wananchi wote,"amesema Bi. Kanyeka.

" Baada ya kusaini mikataba hii na kugawa vitendea kazi katika Halamashauri zote za Mkoa wa Mwanza zitakwenda kuanza kufanya kazi rasmi kuanzia Julai 1, 2023," amesisitiza Bi. Kanyeka



 *Uwekaji wa saini wa mkataba wa utekelezaji* wa kanuni husika ni mwendelezo wa mafunzo yaliyokuwa yameendeshwa hapo awali na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) mnamo Septemba, 2022 kwa baadhi ya watumishi kutoka ofisi za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.