• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Serikali inatambua mchango wa The Desk and Chair Foundation

Posted on: March 21st, 2021

Serikali imesema kuwa inathamini misaada ya kijamii inayotolewa na The Desk & Chair Foundation (TD & CF),katika kuunga mkono juhudi za kuwahudumia wananchi wakiwemo wnye mahitaji maalum.

Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt. Severine Lalika alisema juzi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, kwenye Maadhismisho ya Siku ya Wanawake Duniani,wakati akipokea msaada wa vifaa vya kujifungulia akinamama na baiskeli za walemavu.

Alisema serikali kwa namna ya pekee inaishukuru TD & CF kwa kuunga mkono juhudi zake za kuhakikisha Watanzania wenye mahitaji maalum nao wananufaika na wanajisikia faraja kwa kupata huduma za kijamii kama hizo.

“Nikuhakikishie kwa misaada mnayotoa kama ujenzi wa vyoo kwa shule zetu za msingi na baadhi ya shule za sekondari,serikali tunaithamini sana misaada ya namna hiyo,”alisema Dk. Lalika.

Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Tawi la Tanzania, Alhaji Sibtain Meghjee,alisema msaada huo wa vifaa mifuko 184 kwa ajili ya akinamama wakati wa kujifungua na baiskeli mbili za watu wenye ulemavu umegharimu sh.milioni 6.7.

Alisema walifanya utafiti wao wakabaini akina mama wajawazito wana changamoto ya kukosa vifaa wanapokwenda kujifungua na baada ya kuguswa na changamoto hiyo mwaka huu kwenye madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wameamua kutoa mifuko 184 yenye thamani ya sh.milioni 5.55 vigawiwe bure ambapo mwaka jana waligawa mifuko 280.


Pia baiskeli mbili kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye walemavu zenye thamani ya sh.milioni 1.2 na kufanya idadi ya vyenzo hizo zilizotolewa bure kwa watu hao wenye mahitaji maalum kufikia jumla ya baiskeli 569.


Alhaji Meghjee alisema taasisi hiyo yenye makao makuu nchini Uingereza ilianzishwa mwaka 2003 na Watanzania wenye asili ya Kiasia (wote wazaliwa wa Mwanza) na kwa Tanzania ilisajiliwa na kuanza kazi mwaka 2004.


“Taasisi hii tulianzisha mwaka 2003 ili kusaidia jamii na waalinzishi wote ni wazaliwa wa hapa Mwanza na tunafanya kazi bila kubagua kwa kusaidia jamii katika sekta za afya, elimu na maji,”alisema


Aidha alhaji Meghjee alieleza kuwa taasisi hiyo inajishughulisha na utoaji wa misaada ya kijamii ikigharamia baadhi ya matibabu ya wagonjwa,ujenzi wa vyoo,madarasa,sare za shule na utengenezaji wa madawati.


Pia imechimba visima vifupi na virefu vya maji hasa maeneo ya vijijini na kwenye baadhi ya taasisi za umma pamoja na kutoa vifaa mbalimbali saidizi kwa watu wenye mahitaji maalum.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RAS MWANZA ATAKA UHAMASISHAJI CHAKULA CHENYE LISHE KUONGEZEKA SHULENI

    May 13, 2025
  • RC MTANDA AIPONGEZA BONDE LA ZIWA VICTORIA KWA KUELIMISHA UMMA

    May 13, 2025
  • RC MTANDA ASISITIZA UIMARISHWAJI WA UMOJA NA MSHIKAMANO

    May 12, 2025
  • SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI MWANZA

    May 10, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.