• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Serikali yatenga Shilingi Trilioni 1.15 kwa ajili ya Elimu ya awali na Msingi nchini

Posted on: January 22nd, 2023


Jumla ya Shs Trilioni 1.15 zimetengwa na Serikali mwaka huu Kwa ajili ya kuboresha Elimu ya awali na Msingi nchini huku kipaumbele kikiwekwa cha kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na uimarisharishaji wa miundombinu Shuleni.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Angella Kairuki amesema hayo leo Mkoani Mwanza wakati wa kufunga kikao kazi cha Tathmini ya uboreshaji elimu mwaka 2022-23 na mkakati wa mwaka huu wa mabadiliko kwenye Sekta hiyo kilichowakutanisha walimu wa Msingi na Sekondari, na Maafisa Elimu wa ngazi zote Mkoani humo,amesema mpango huo utaondoa adha yote ya msongamano wa wanafunzi waliozidi idadi ya 60 darasani na kujengwa madarasa mengine.

"Huu ni mpango wa miaka mitano ambapo Shule zote zenye wanafunzi wa zaidi ya 1500 zitajengwa Shule nyingine ambapo jumla ya Shs bilioni 250.6 zitatumika kujenga madarasa 9000 nchi nzima"amesema Mhe Waziri.

Ameongeza kuwa kata 3900 zilizopo nchini zitanufaika na kupata shule moja za Sekondari kutokana na fedha nyingine iliyotengwa shs Trilioni 1.2 na kusisitiza Serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kwa vitendo  kuiboresha sekta hiyo ili watoto wote wapate elimu bora na wasome katika mazingira rafiki.

" Mhe Rais ameonesha namna alivyopania kumletea maendeleo mwananchi kwa kutoa kiwango kikubwa cha fedha,wajibu wetu sasa sisi walimu na tuliopewa dhamana ya uongozi ni kumuonesha kiongozi wetu wa nchi matokeo chanya kwenye elimu ukiwemo ufaulu mzuri Msingi na Sekondari na mwamko wa juu wa watoto kuandikishwa shule".Amehimiza Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu,Dkt.Charles Msonde.

"Mkoa wa Mwanza tumeendelea na mkakati wa kuboresha Elimu na kufanikisha kukamilisha ujenzi wa madarasa kwa wakati kwenye Wilaya zote japo changamoto iliyopo ni uhitaji wa jumla ya walimu 9442. Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Hassan Masala.

"Tumepokea na tutaifanyia kazi miongozo yote iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt.Charles Msonde inayotaka kuja na matokeo chanya katika Maendeleo ya Sekta hiyo Mkoani kwetu".Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza,Martine Nkwabi

Kikao kazi hicho pia kimewashirikisha Wakuu wote wa Wilaya, na Wakurugenzi wa Halmashauri kutoka Mkoani Mwanza

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. July 29, 2022
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2022 July 03, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI ICAP October 21, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC Malima ataka adhabu kali na marekebisho ya Sheria za barabarani dhidi ya wanaosababisha ajali kwa uzembe

    March 17, 2023
  • Tupo katika mchakato wa Katiba mpya-Mhe.Dkt.Ndumbaro

    March 17, 2023
  • Miaka miwili ya Rais Samia madarakani,Mwanza yajivunia kasi ya miradi ya maendeleo

    March 15, 2023
  • Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt.Abubakar Zuber akemea maovu ndani ya Jamii

    March 15, 2023
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 33180, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.