• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Serikali Yawataka wakulima kujikita katika kilimo cha pamba

Posted on: January 22nd, 2020


Serikali  imezindua rasmi   msimu  wa kilimo cha zao la pamba mkoani Mwanza huku ikitangaza kufanya operesheni ya  kuwasaka vijana wanakaa vijiweni na kucheza michezo ya kubahatisha na kuwataka kufanya kazi.


Akizindua msimu huo   kwa kupanda mbegu kwenye shamba  darasa la kikundi cha Jikomboe katika Kijiji cha Gunge  Kata ya mwaniko, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Mhe. Juma Sweda alisema  kuanzia sasa hataki kuona wananchi wa kuzurula mitaani au kwenye baa.


Alisema kuanzia sasa anataka kuona  wananchi ndani ya wilaya hiyo wakiwa  mashambani  na atakayekamatwa na kikosi cha operesheni ya kuwasaka wazembe mitaani  na kupangiwa kazi ya kufanya ndani ya jamii kwa siku nzima bila malipo.


Mhe.Sweda alisema Serikali imejipanga kusimamia zao la pamba ili msimu wa 2019/2020  wakulima waweze kuvuna pamba yenye ubora wa kushindana soko la kimataifa ambapo aliwahakikishia uhakika wa soko.


“Kama mlivyoshuhudia nimezindua mimi kama Mkuu wa wilaya msimu wa upandaji mbegu za pamba, sasa kuanzia sasa kila mmoja aingie shambani na kuanza kupandikiza mbegu kwenye shamba lake, wito wangu kwa  bwana shamba wa kila kata watoke ofisini na kwenda kwa wakulima ili kuwaelekeza namna ya kupanda kwa kufuata kanuni bora za kilimo cha pamba na itakapofika hatua ya kupalilia wafanye hivyo bila kusahau kupalilia mashamba yao.


“Naomba wananchi wasisahau mazao ya chakula, ni muhimu kuwa na zao la biashara na chakula hivyo yote kwa pamoja yanapaswa kwenda sambamba,naomba niwadokeze kuwa wakulima wengi wanashindwa kupata mazao mengi kwa sababu tunalima kienyeji, sasa mwaka huu nataka Misungwi tuwe mfano katika zao la pamba lenye ubora,”alisema Mhe.Sweda.


Kwa upande wa Afisa Kilimo na Umwagiliaji wa Misungwi, Majid Kabyemelwa alisema  shamba darasa la kikundi cha Jikomboe  lenye hekari  mbili limekuwa mfano kwa wakulima wote ndani ya Wilaya ya Misungwi ambapo mwaka jana walivuna kilo 450 kwa hekari moja.


“Mwaka huu tumejipanga kulima hekari 15,940 ndani ya Wilaya ya Misungwi kwa msimu wa 2019/2020 ambapo nitahakikisha nawasimamia wataalaamu wangu kwenda mashambani kutoa elimu kwa wakulima ili tuvune pamba yenye ubora wa hali ya juu, naomba niwahakikishie hadi sasa hakuna mkulima anayedai fedha za pamba kwani zote zimeletwa,”alisema.


Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Jikomboe, John Lugomeji alisema wamepata mafanikio makubwa kutokana na kilimo cha pamba ambapo baadhi ya wanachama wameweza kujenga nyumba za kisasa,kusomesha watoto, kuanzisha miradi ya biashara na kununua vitendea kazi vya kilimo.


“Pamoja na mafanikio hayo lakini kuna changamoto imejitokeza ya kuchelewesha malipo ya pamba, ndio maana ukichunguza kwa undani baadhi ya wakulima wamekataa kuanza maandalizi ya kuandaa mashamba yao na kudai kuwa uhakika wa soko haupo, hivyo tunaiomba Serikali kuleta wanunuzi wengi na sio mmoja,”alisema.


Aidha Bwana Shamba wa Kata ya Mwaniko, Sosteness Wabukoba alisema msimu wa 2018/2019, Serikali iliwalipa wakulima wa pamba Sh. milioni 60 katika vituo vya Nyasato, Gunge na Mwaniko.

Hata hivyo aliwaomba wakulima kuzingatia kanuni 10 za kilimo cha pamba msimu huu akisisitiza kuanzia sasa atakuwa  anazunguka katika mashamba kwa ajili ya kutoa elimu ya namna ya kupanda, kupalilia,kumwagilia dawa na mambo mengine kadri itakavyohitajika.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.