• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Serikali yazipongeza Taasisi za Kidini kwa Huduma Bora kwa Jamii

Posted on: July 9th, 2022

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike amezipongeza Taasisi za kidini ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za kijamii ikiwemo Elimu hatua ambayo imeongeza kasi ya Maendeleo nchini.

Ametoa pongezi hizo leo wakati wa Mahafali ya kuwaaga Umoja wa Wanafunzi Wakatoliki (TMCS) yaliyofanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Kanda ya Bugando.

"Serikali itaendelea kuthamini mchango wenu, tangu kuanzishwa kwa Vyuo hivi vimewanufaisha Watanzania wengi na Serikali kwa ujumla kwani watu wenye afya ni mtaji muhimu wa Maendeleo kwa Taifa." amesema Ngusa.



Samike, amewakumbusha Wahitimu hao kuendeleza Taswira ya Ukatoliki waliotoka nayo vyuoni ili kuwa mfano wa kuigwa ndani ya Jamii huku wakibuni mbinu mbalimbali za kujiajiri wenyewe kutokana na Serikali kutoa fursa nyingi za mikopo.

Aidha, amewataka Wataalamu wa dawa kuleta mageuzi chanya  watakapoajiriwa kutokana na changamoto iliyopo sasa ya dawa nyingi kuchina kwenye Vituo vya afya hali inayosababishwa na uagizaji usiozingatia takwimu sahihi.

Mlezi wa Umoja wa Wanafunzi hao Padri Renatus Mashishanga amesema wamekuwa na mafanikio mbalimbali yakiwemo kufanya matendo ya huruma kwa kuwatembelea na kuwapa mahitaji muhimu wafungwa kwenye Gereza la Butimba na watoto waishio katika mazingira magumu.

Pia, Katibu Tawala amewakumbusha  Wahitimu hao kushiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika nchini kwa wale walio ndani ya mipaka ya Tanzania mnamo Agosti 23 mwaka huu.

Mahafali hayo ya Wahitimu Wanafunzi Wakatoliki yamewajumuisha wanaosomea Udaktari, Uuguzi, Ufamasia, Utaalamu wa Maabara, na Utaalamu wa Viungo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.