• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Shilingi milioni 500 zatolewa na Serikali kutafiti ugonjwa wa Saratani Kanda ya Ziwa

Posted on: September 13th, 2022


Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amezindua Jengo la Wodi ya Saratani katika Hospital ya Rufani ya Bugando ili kupunguza vifo vitokanavyo na saratani kwa kuwa wagonjwa wengi watapata matibabu kwa ukamilifu huku serikali ikitoa kiasi cha shilingi billion 3.1 kwa ajili ya ununuzi wa mashine moja ya mionzi.

Akizindua Jengo hilo Mhe. Dkt Mpango amesema takwimu zinaonyesha ugonjwa wa saratani unaua  watu wengi duniani huku nchini kukiwa na ongezeko la ugonjwa huo ambao unawapata  watu elfu 42 hasa Kanda ya Ziwa ambapo Serikali imetoa millioni 500 kwa ajili ya kusaidia utafiti wa ugonjwa huo unaofanywa na madaktari bingwa wanaotoka katika hospital hiyo.


Amesema Serikali inaendesha harakati za kupambana na ugonjwa huo huku elimu za kuondokana na viatarishi  vinavyochangia kuondokana na hatari hizo zikiwemo ufanyaji mazoezi ,umuhimu wa chakula,kupunguza matumizi ya pombe kutasaidia kukabiliana tatizo hilo.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi wa Ujenzi wa Jengo la  Wodi ya Saratani Mkurugenzi Mtendaji wa hospital hiyo Dkt.Fabian Massaga amesema tatizo la saratani bado ni kubwa Kanda ya Ziwa watu elfu 45 wanaugua saratani hivyo iliwalazimu kuchukua sampuli za damu katika mikoa nane ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kufanya utafiti wa chanzo cha ugonjwa huo.

Ameongeza kuwa, mradi huu ulianza Septemba 1 mwaka 2020, kwa sasa umefikia asilimia 96, kazi zilizobaki ni za umaliziaji, ambazo zitakamilika hivi karibuni pia jengo hilo lenye ghorofa tatu lina ukubwa wa mita za mraba 4,100.

Aidha, matibabu ya Saratani katika hospitali  hiyo yalianza Mwaka 2009 ambapo dawa za kemikali (chemotherapy) zilikuwa zinatolewa , kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa wa Saratani, hospitali ya Bugando kwa kushirikiana na Serikali na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Kiatomiki (International Atomic Energy Agency)  waliandaa mpango wa kupanua huduma za matibabu ya Saratani katika hospitali hiyo.

Vilevile mpango huu ulikuwa wa awamu mbili awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa jengo maalumu la kusimika mashine za matibabu ya mionzi ambalo lilikamilika mwaka 2015 na kuanza kutumika mwaka 2017 baada ya ununuzi na usimikaji wa mashine za matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi huku awamu ya pili ilihusisha ujenzi wa jengo la kulaza wagonjwa wa saratani (oncology ward).

"Hospitali ya Bugando ni hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa, kanda ambayo ina watu zaidi ya Milioni 17 katika Mikoa yote 8 inahudumia mikoa yote na baadhi ya Mikoa ya Kanda ya Kati na Nyanda za Juu Kusini jengo hili lina umuhimu kwa sababu idadi ya wagonjwa wa Saratani watakaopata matibabu hapa itaongezeka"alisema Dkt.Massaga.

Amesitiza kuwa Huduma zinazotolewa kwenye jengo hili ni matibabu kwa njia ya mionzi na dawa za kinyuklia huduma hizo zitatolewa kwenye sakafu ya ardhini, huduma ya kuona wagonjwa wa nje  na matibabu ya utoaji wa dawa kwenye sakafu ya kwanza, pamoja na huduma ya kulaza wagonjwa wodini  kwenye sakafu ya pili na ya tatu, ambapo jengo hilo linakusudiwa kua na vitanda vya wagonjwa 120, pamoja na huduma zingine zinazo husiana na matibabu ya ugonjwa wa saratani.

Aliongeza kuwa, Mradi huu hadi kukamilika kwake unabajeti ya kiasi cha Sh. bilioni 5.4, hadi sasa mradi huu umesha tumia takribani kiasi cha Sh  bilioni 4.7 katika kununua vifaa vya ujenzi, kumlipa mkandarasi mjenzi na Mhandisi mshauri.

Hata hivyo, ili huduma zilizo kusudiwa ziweze kutolewa kwa ufanisi kama zilivyo kusudiwa upo uhitaji wa vifaa vya ujenzi, miundombinu ya kuzuia mionzi, samani za kutumika kwenye jengo hili na vifaa tiba kwa ujumla wa mahitaji hayo ni takribani Sh. bilioni 12 ambayo yameshawasilishwa Wizara ya Afya.

"Matarajio yetu mradi utakapokamilika utakuwa na faida nyingi ikiwemo kuongezeka kwa ubora wa huduma kwa wagonjwa wa saratani wanaopata matibabu hapa kwakuwa watakuwa na  sehemu nzuri na ya kisasa ya kupumzika wakati wanapata matibabu,kupungua kwa gharama za malazi hasa kwa wagonjwa wanaotoka mikoa ya mbali waliolazimika kupanga kwenye mahoteli nje ya hospitali wakati wa kupata matibabu." Alieleza  Dkt. Massaga.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Mhe.Adam Malima ameishukuru sana serikali ya awamu ya sita inayoogozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan  kwa kudumisha ushirikiano na wadau huduma hii inamafanikio makubwa kwa wananchi kwa sababu zinapunguza uzito wa wananchi kwenda mbali kutafuta matibabu kuwepo kwa huduma hii ni mkombozi kwa kwa wananchi.

Aliongeza kuwa matarajio ya Mkoa wa Mwanza ni kuwa kitovu cha huduma za afya Kanda ya Ziwa na Magharibi pia tutadumisha uhusiano na wadau na taasisi za afya ili kuwepo kwa huduma bora na zenye tija kwa jamii.

Kwa upande wake, Mhashamu baba Askofu wa Jimbo la Kigoma na Mwakilishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhe. Joseph Mlola  akitoa neno wakati wa Misa ya Uzinduzi wa Jengo  hilo amesema wagonjwa watakaokuja kutibiwa katika Jengo la Saratani wapate uponyaji wa haraka na amewashukuru wote waliofanikisha ujenzi wa jengo hilo hadi kukamilika kwani limeleta amani,furaha na faraja kwa wagonjwa.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.