• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

SHIMMUTA Kufanyika Mwanza

Posted on: September 12th, 2019


Kikao cha wadau wa michezo kimefanyika mapema hii leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  wa Mwanza, lengo la kujadili maandalizi ya Bonanza la michezo lililoandaliwa na shirikisho la michezo la mashirika ya Umma Taasisi na makampuni binafsi Tanzania (SHIMMUTA) lililopangwa kufanyika tarehe Octoba 12 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa CCM Kirumba.

Akizungumza katika kikao hicho  Afisa michezo Mkoa wa Mwanza, James William amesema kama mkoa wa Mwanza umeyakubali mashindano haya ya Bonanza kwani yatafungua mlango wa michezo kwa mashirika, viwanda na makampuni pia itakuwa na faida kwa wafanyakazi.

“Sisi Mkoa wa Mwanza tumeyakubali na tukasema uwe mlango wa michezo kwa mashirika, viwanda na makampuni na zipo faida za kuwa na michezo kwa wafanyakazi kama kujenga afya kutokomeza baadhi ya magonjwa kama magojwa ya moyo na kisukari,” Alisema William.

Aidha, William amesema kuwa bonanza hilo la michezo limepokelewa kama moja wapo ya fursa ya  kujenga mahusiano nakukuza uchumi katika mkoa wa Mwanza.

“Ninaamini wageni wataokuja katika kushiriki katika bonanza hili watafanya hoteli zipate watu, vituo vya petrol vitapata watu na mwisho wa siku mzunguko wa uchumi utakuwa umepatikana Mwanza.’’Alisema William.

Naye mwenyekiti wa Shirikisho la michezo la mashirika ya umma taasisi na makampuni binafsi Tanzania,(SHIMMUTA), Khamis Mkanach amebainisha kuwa bonanza hilo litahusisha michezo mbali mbali na kuomba mashirika mbalimbali  kujitokeza kwa wingi kushiriki..

‘’Bonanza hili la michezo litajumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu,mchezo wa kuvuta kamba ,mchezo wa kufukuza kuku, mchezo wa bao, mchezo wa karata pamoja na mchezo wa draft.’’Alisema Mkanach.

Hata hivyo, Mkanach ameweza kuweka wazi kuwa zitakuwepo zawadi mbali mbali kwa wale watakaoibuka washindi katika bonanza hilo la michezo.

‘’wataoibuka washindi katika bonanza hilo watapata zawadi mbali mbali zikiwemo medali,vikombe pamoja na zawadi ya mpira kwa mchezaji atayefunga hat trick katika mchezo wa miguu’’.Alisema Mkanach

Pamoja na hayo Mkanach ametoa wito kwa wadau hao kuweza kutangaza bonanza hilo, pia ameweza kutoa wito kwa makampuni mbali mbali kuweza kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika bonanza hilo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.