• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Shirikisho la Walimu Makada wa CCM Mwanza waiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita kwa kufanya shughuli za kijamii

Posted on: October 6th, 2022

Shirikisho la Walimu Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza linatarajia kufanya shughuli za kijamii katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Shirikisho hilo tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti Jackson Kadutu, Katibu wa Shirikisho Mwalimu David Sulube amesema katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita wameamua kutoa Msaada kwa Mama na Mtoto kwenye Hospitali ya Buzuruga wenye thamani ya Tshs. Milioni 2 siku ya jumamosi ya tarehe 08 Oktoba, 2022.

Aidha, mwalimu Sulube amesema kuwa katika maadhimisho hayo wanatarajia pia kupanda Miti elfu kumi kwenye wilaya zote za Mkoa huo ambapo uzinduzi Rasmi wa shughuli hiyo utafanywa katika shule ya Sekondari Lugeye iliyopo wilayani Magu siku ya ijumaa ya tarehe 07, 2022.

Amesema, kwenye siku hiyohiyo ya ijumaa kutakuwepo na ugawaji wa taulo za kike zenye thamani ya Tshs. Milioni mbili na laki tano kwa watoto 300 wa kidato cha tano na sita katika shule hiyo kwa awamu ya kwanza lakini pia zitagawiwa taulo hizo kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya Sekondari Buhongwa.

"Siku ya jumamosi shirikisho tutakuwa na Shughuli nyingine muhimu sana ya kijamii ya uchangiaji wa damu na utoaji wa misaada kwa mama na Mtoto," amefafanua Mwalimu Kaligiwa.

Shirikisho la Walimu wa Chama Cha Mapinduzi limeipongeza Serikali kwa kutekeleza Ilani ya CCM ibara ya 84 inayotaka  kuboreshwa kwa huduma za afya hususani Mama na Mtoto kwani baada ya kuboresha vifaa tiba kwenye Hospitali ya Buhongwa kumekua na ongezeko la wamama wanaojifungua hadi 600 kwa mwezi kutoka 200 siku za nyuma.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.