SUNGUSUNGU DAY YAFANA MWANZA, RAIS SAMIA ASIMIKWA UTEMI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo juni 20, 2025 amezungumza na jeshi la jadi Sungusungu zaidi ya elfu 30 katika viwanja vya CCM Kirumba ambapo amesimikwa Utemi na jeshi hilo kama ishara ya kumuunga mkono katika kulinda amani nchini.
Akizungumza na kundi hilo pamoja na mengine Mhe. Rais amewashukuru kwa kumsimika Utemi na akawataka kuendelea kulinda amani na kwa makundi ya boda boda kufuata sheria za usalama barabarani ili kulinda uhai wa watumiaji barabara kwa kuwaepusha na ajali zinzozuilika.
“Maendeleo yaliyofanyika nchini yanahitaji kulindwa na kutunzwa kama miundombinu ya maji, shule, hospitali, umeme na kwakua ninyi ndio walinzi kwenye jamii naomba tuendelee kuwa msitari wa mbele kwenye kuitunza na nawaomba mkabebe sera za serikali kama chanjo ya mifugo ili wafugaji wakaitumie vema.”
Vilevile, ametoa rai kwa makundi mbalimbali nchinu kuunda vikundi na kurumia fursa za mikopo ya aslimia 10 ili kufanya biashara na kukuza uchumi wao na akawataka maafisa kwenye halmashauri kuwasaidia kufanikisha hilo hususani ujazaji sahihi wa fomu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amempongeza Mhe. Rais kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuongoza serikali ya awamu ya sita na amemuahidi kwa niaba ya mikoa ya kanda ya ziwa akiwa mwenyekiti wa wakuu wa Mikoa kuwa jeshi hilo na jadi litalinda amani.
Aidha, pamoja na shukurani hizo Mhe. Mtanda ametumia fursa hiyo kuwasilisha zawadi ya Mkoa wa Mwanza kwa Mhe Rais ambayo ni ng’ombe kumi waliotolewa na makundi mbalimbali
Akitoa salamu za Sungusungu kutoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara na Mwanza ndugu Richard Bundala amesema wanayo furaha kuazimisha miaka 42 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la jadi na kwamba wanaendelea kulinda amani ya nchi kwa kuhamasisha jamii kuacha tabia hatarishi kama wizi wa mali.
“Mwanzoni mwa miaka ya 1980 kulishamiri wizi wa mifugo na mali ndipo wazazi wetu wakaanzisha jeshi la jadi lililohakikisha linakomesha kadhia hiyo ambayo tunaendeleza na tunatoa wito kila raia kulinda mali ili kuongeza msukumo wa kujihusisha na uzalishaji maji.” Amesema Bundala.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.