• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

TASAF yawa mkombozi kwa wasichana Mabuki, yawajengea Shule ya bweni

Posted on: August 4th, 2023

*TASAF yawa mkombozi kwa wasichana Mabuki, yawajengea Shule ya bweni*


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala bora, Mhe. George Simbachawene ameipongeza Serikali ya Wamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Fedha za Miradi nchini ikiwemo Ujenzi wa shule Maalum ya Wasichana Mwanangwa katika Kata ya Mabuki wilayani Misungwi.


Waziri Simbachawene ametoa pongezi hizo leo Agosti 04, 2023 wakati akikagua Ujenzi wa  Shule ya Bweni ya Wasichana Mwanangwa chini ya Mradi wa kupunguza Umasikini awamu ya Nne kwa zaidi ya Milioni 138.8 uliounganisha vijiji vitano vya Mwanangwa, Ndinga, Mwagagala, Mhungwe na Lubuga vyenye jumla ya wakazi 15,252.

Amesema, kutoa fedha nyingi kiasi hicho kwa ajili ya kusogeza Elimu karibu ni uzalendo na ameonesha kuwajali watoto wa kike ambao awali wamekua wakitembea umbali mrefu na wamekua wakikumbana na vishawishi mbalimbali vilivyopelekea wakati mwingine kupata vishawishi na kupata Ujauzito na kukatisha masomo.

Aidha, amewaagiza TASAF na Halmashauri ya Misungwi kushirikiana kujenga wigo kwenye shule hiyo pamoja na njia za kupita wanafunzi kutoka Jengo moja kwenda jingine ili maeneo ya shule hiyo yawe nadhifu na yenye kuwapa mazingira ya usiri wanafunzi hususani wawapo kwenye maeneo ya bwenini na vilevile amewataka kupanda miti ili kulinda mazingira.

Naye, Mhe. Alexander Mnyeti Mbunge wa Jimbo la Misungwi ameishukuru Serikali kwa niaba ya wananchi kwa kuleta fedha kwenye miradi na akabainisha kuwa wilayani humo kuna Shule mbili mpya zinajengwa na kwamba kwenye upande wa Afya, Maji, Miundombinu ya barabara na sekta zingine miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa.

"Vijiji  hivi kwa pamoja viliafikiana shule kujengwa katika Kijiji cha Mwanangwa na kuibua miradi 10 yenye Majengo 6 Katika Mwaka wa kwanza wa Utekelezaji 2022 ikiwa ni Ujenzi wa Bweni la Wasichana, Bwalo, Madarasa 4, Ofisi na Matundu 12 ya vyoo, Jengo la Utawala na Maabara ya Biolojia na Kemia pamoja na nyumba ya Walimu 1 (2kwa 1)". Gloria Bunane Mratibu wa TASAF Misungwi.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.