• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

TEMESA Yashauriwa kuongeza Malengo,udhibiti na ukusanyaji mapato

Posted on: July 31st, 2019


Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeushauri Wakala wa Vivuko na Umeme (TEMESA) kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuimarisha udhibiti wa mianya ya upotevu  mapato iweze kujiendesha badala ya kutegemea ruzuku ya serikali.

Pia  TEMESA kwa kushirikiana na  uongozi wa TASAC na vyombo vya usalama waunde kamati itakayoshughulikia utatuzi wa changamoto ya shughuli za uvuvi zinazofanyika kwenye njia za vivuko na kuielimisha jamii madhara yanayoweza kuathiri vyombo vya usafiri wa majini.

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC, Profesa Thadeo Satta kwa niaba ya wajumbe wa bodi hiyo baada ya kutembelea na kukagua vivuko vya MV. Mwanza na MV. Misungwi vinavyotoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya Kigongo, wilayani  Misungwi na Busisi, Sengerema.

Alisema ili wakala huo ujiendeshe wenyewe,  uongeze juhudi kwenye ukusanyaji wa mapato na kudhibiti mianya ya upotevu ili fedha za ruzuku zinazotolewa na serikali zikahudumie sekta zingine.

Mwenyekiti huyo wa bodi ya TASAC alisema, vivuko vya TEMESA vinatoa huduma kwa wananchi na havifanyi biashara ili kupata faida ambapo serikali imekuwa ikitoa ruzuku inayotumika kujenga vivuko vipya na ukarabati wa vivuko vyenye hitlafu na uchakavu wa mitambo, hivyo TASAC imeridhishwa na bajeti ya wakala huo wa vivuko na ufundi wa umeme.

  “TASAC ipo kwa ajili ya kuangalia masuala ya kiusalama na hapa kaimu meneja wa TEMESA ameeleza changamoto ya shughuli za uvuvi zinazofanyika kwenye njia za vivuko zinaathiri na zinahatarisha usalama wa abiria na vivuko vyenyewe.Tunaelekeza waunde kamati ya utatuzi wa tatizo hilo kwa kuwaelimisha wavuvi na jamii ili kulinda usalama wa abiria na vyombo vyenyewe,”alisema Profesa Satta.

Alisema serikali imeweka vyombo hivyo kuwahudumia wananchi kutoka upande mmoja kwenda ng’ambo ya pili na ili kunusuru maisha ya watumiaji wa vivuko wavuvi waache kufanya shughuli zao kwenye njia za vivukokwani wanaisababishia serikali hasara.

Awali Kaimu Meneja wa TEMESA Mkoa wa Mwanza Abdallah Atiki, alisema wakala huo unajiendesha kwa kutumia mapato ya ndani na mwaka huu imetenga bilioni 16 kwa jili ya kuhudumia vivuko vyote nchini na wameimarisha usalama na mifumo wa ukusanyaji wa maduhuri ya serikali.

Alisema mwaka 2018/2019  kwa kutumia vikosi vyake vya ufundi,walifanya matengenezo kinga kwa vivuko na kuondoa vipuri chakavu  na kuviwezesha kuwa salama, kutoa huduma bora za uhakika kwa saa 24  na usalama wa abiria na mizigo.

Atiki alisema wanakabiliwa na changamoto ya watu binafsi kusafirisha abiria kwa kutumia mitumbwi na injini isiyo salama katika baadhi ya maeneo yanayohudumiwa na vivuko vya TEMESA, wavuvi kuendesha shughuli zao (kutega nyavu) kwenye njia za vivuko.

“Tuna changamoto ya vyombo binafsi visivyo salama kusafirisha abiria kwenye maeneo yenye vivuko mbali na kuhatarisha usalama wa abiria  vinachangia kupunguza mapato.Pia zana za uvuvi kutengwa kwenye njia za vivuko zikinasa kwenye mifumo ya injini zinahatarisha usalama na uharibifu wa chombo,” alisema.

Kwa mujibu wa meneja huyo hadi mwaka 2018/2019 walikusanya maduhuri ya serikali sh. bilioni 5.7 ambapo makadirio ya bajeti ya mwaka  2019/2020 ni kukusanya sh. bilioni 7  lakini kwa hali ilivyo wanaweza kukusanya bilioni 6 chini ya lengo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.