• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

TRA Yajipanga kukusanya mapato maoneaho ya TCCIA Mwanza

Posted on: August 20th, 2019


Mamlaka  ya Mapato Tanzania (TRA) imewaonya   washiriki wa maonyesho ya  14 ya Afrika Mashariki   yanayotarajiwa kuzinduliwa Agosti 30, mwaka huu mkoani Mwanza, kwamba atakayekiuka sheria na taratibu  atakumbana na adhabu ya kifungo au faini   inayofikia Sh milioni  nne.


Onyo hilo limekuwa ikiwa ni siku moja baada ya Chemba   ya Wafanyabiashara,wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) kutangaza siku ya ufunguzi wa  maonyesho ya  14 ya Afrika Mashariki   yanayotarajiwa kuzinduliwa Agosti 30 na kufikia tamati Septemba 8, mwaka huu huku mataifa nane na kampuni 300 kuthibitisha kushiriki.


Akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake, Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Joseph Mtandika alisema wamejipanga kuhakikisha  kila mshiriki wa maonyesho hayo anazingatia  sheria  na taratibu zilizopo  zikiwa za kutoa  na kudai stakabadhi ya  mashine ya elekitroniki ( EFD) iliyo na  gharama halilsi  ya kile alichokinunua au kuuza.


Mtandika alisema  sheria  zinamtaka mtu yeyote ambaye mauzo yake kwa mwaka yanafikia Sh  milioni  14  na kwa siku Sh 39,000 anapaswa kuwa na mashine ya EFD ambapo aliainisha kwamba atakayenunua kitu bila kudai stakabadhi adhabu yake ni kifungo au kulipa faini inayoanzia Sh 30,000 hadi Sh milioni 1.5.

“Adhabu kwa muuzaji ambaye atashindwa kutoa stakabadhi kwa mteja wake, akikamatwa  atalazimika kulipakati ya Sh milioni tatu hadi nne kulingana na uzito wa kosa unaoendana na kile alichokiuza, tunaomba wafanyabiasha waache visingizio juu ya suala la kodi.

“Kama mashine ya EFD imekuharibikia ukiwa katika maoenyesho hayo unatakiwa kutoa taarifa TRA  na yule aliyekuuzia hiyo mashine, pia  vile vitu ambavyo  ataendelea kuviuza  wakati akisubiria  mashine ile kutengenezwa ni lazima atoe stakabadhi ya kitabu cha mkono ambapo sisi kama TRA tutapita kukagua ili kujiridhisha.


“Baada ya mashine kurejeshwa anatakiwa taarifa zote zilizopo kwenye stakabadhi ya kitabu cha mkono aziingize kwenye mashine ili kuweka kumbukumbu sawa, kama TRA tutashiriki na tutatembelea washiriki wote na kuwapa elimu, pia kwa wale ambao watakuwa na uwezo wa kuingia kwenye tovuti zetu watapata kila kitu,”alisema.

Mtandika alisema waonyeshaji au wauzaji wa bidhaa  wanatakiwa kuwasilianana  TRA  au mawakala wa kusafirisha mizigo (clearing and fowaring arget) ili kupata taarifa na a taratibu za kuingiza mizigo kutoka nje ya nchi zikiwamo  ushuru wa forodha, ushuru wa bidhaa.


Hata hivyo meneja huyo aliwaomba  viongozi wa TCCIA   kuwaelimisha washiriki wa maonyesho hayo ili Serikali isiweze kupoteza mapato.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Dk. Elibariki Mmari, alisema  bidhaa zitakazoonyeshwa katika maonyesho hayo ni  kundi la vyakula,  kilimo na vinywaji,  nguo,  ngozi, vifaa vya viwandani, ujenzi, umeme, pembejeo za kilimo, urembo, mbao za samani, uhandisi na huduma za kibiashara.

Alisema maonyesho hayo yatafanyika  katika viwanja vya jengo la Biashara la Kimataifa la Ricky City Mall jijini Mwanza ambapo nchi za Kenya, Uganda,Rwanda, Indonesia, India, Syria, China na kampuni 300  zimethibitisha kushiriki ambapo yatafunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa  Agosti 30 na kufunga Septemba 8, mwaka huu.

Dk. Mmari alisema miongoni mwa fursa zitakazopatikana kutokana na maonyesho hayo ni kuimarisha mtandao wa masoko na usambazaji bidhaa,  kampuni za Tanzania kujifunza na kutanua wigo wa biashara kwa kutumia  makubaliano ya kibiashara ya kimataifa.

Vile vile alisema kufanyika maonyesho hayo yanatoa mchango kwa vitendo katika kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli kuifanya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati ifikipo 2025 sambamba na kuimarisha mtengamano wa soko la pamoja la Afrika Mashariki.



Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.