• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

TUMUENZI BWIRE KWA KUENDELEZA MICHEZO MWANZA:RC MTANDA

Posted on: January 31st, 2025

TUMUENZI BWIRE KWA KUENDELEZA MICHEZO MWANZA: RC MTANDA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda  amewaongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa mkurugenzi wa kituo cha michezo cha Alliance Sports Academy, Marehemu James Bwire na kuwakumbusha njia pekee ya kumuenzi ni kuyatenda kwa vitendo mema yote aliyotenda ikiwemo kuendeleza michezo.

Akizungumza leo Januari 31,2925 wakati wa kutoa salamu za rambirambi nyumbani kwa marehemu Nyakato-mahina wilayani Nyamagana,Mkuu huyo wa Mkoa amesema enzi za uhai wake marehemu ametoa mchango mkubwa wa kuendeleza michezo na taaluma ya elimu kupitia vituo vyake vya michezo na shule,hivyo juhudi hizo hazina budi kuendelezwa.

"Marehemu Bwire nimebahatika kumfahamu ni mtu aliyekuwa na msimamo katika kile alichokuamini,timu yake ya Alliance hata pale ilipoanza kuyumba hakukata tamaa zaidi ya kusimama kidete kuipigania,"Mtanda.

Mtanda ameendelea kubainisha maendeleo ya michezo hayaji kimiujiza bali yanahitaji moyo wa kujitoa,uvumilivu na upendo pia mfano ambao hauna budi kuigwa aliyotuwachia Bwire.

"Leo tumeona ushuhuda wa baadhi ya wanafunzi na wanamichezo waliosoma shule za Alliance ambao sasa wamekuwa na mchango mkubwa katika Taifa wakiwemo wachezaji Israel Mwenda,Athanas Mdamu, Mapinduzi Balama,"Mkuu wa Mkoa

Aidha Mhe.Mtanda ametoa pole kwa familia ya Bwire kwa kuondokewa kwa mpigo  mpendwa wao na mama yake mzazi na kuwaahidi kuendelea kushirikiana nao katika raha na shida.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa mapema leo asubuhi ameshiriki katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa mrakibu mwandamizi wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza Dkt.Aloyce Kessy.

Akizungumza mara baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye viwanja vya Polisi Mabatini,Mtanda amesema marehemu enzi za uhai wake alitumia muda wake mwingi kupambania afya za wananchi wakiwemo askari wenzake,na kuwaomba waendelee kumuombea apumzike kwa amani peponi.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.