• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Tunahitaji wakina Mbogo wengi kwa ajili ya Maendeleo - Mongella

Posted on: October 22nd, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amepokea vyumba 2 vya madarasa  Shule ya Msingi Bukandwe  na matundu 12 ya vyoo na chumba maalumu kwa ajili ya  kuhifadhia  taulo za kike  kwa wanafunzi wa kike, vilivyojengwa na Kampuni ya Mbogo Mining & General Supply Ltd kkwa ajili ya wanafunzi wa Shule hiyo.

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Mhe. Mongella amesema Kampuni hiyo imefanya mambo makubwa ya maendeleo kwa ajili ya Wilaya hii.

"Tunahitaji wakina Mbogo wengi ili kuleta maendeleo ya shule zetu na Mkoa kwa ujumla,"alisema Mongella.

Awali akiongea  wakati wa kukabidhi majengo hayo Meneja wa Usalama na Afya mahala pa kazi wa Kampuni hiyo  Leone Eusebi Salekwa  amesema Kampuni hiyo imetoa ajira kwa watanzania 63 na wamewapa kipaumbele wakazi wa Ihayabuyaga.

"Ujenzi wa chumba cha darasa Shule ya Msingi Bukandwe umegharimu Shilingi Milioni 45, wakati ujenzi wa matundu ya 12 vyoo  na chumba maalumu cha kuhifadhia taulo za kike pamoja na taulo 100 umegharimu  milioni 10.75," alisema Salekwa.

Aidha Salekwa ameongeza kuwa pamoja na makabidhiano hayo wamejenga pia chumba kimoja cha darasa katika shule ya msingi Bukandwe kilichogharimu Shilingi  milioni 45, ujenzi wa matundu 12 ya vyoo na chumba maalum cha kuhifadhia taulo za kike pamoja na taulo 100 za kike ambazo zilikabidhiwa leo.

Tumejenga pia chumba cha darasa shule ya msingi Ilendeja chenye thamani ya sh.milioni 45,ukarabati wa choo cha walimu  shule ya msingi Ilendeja kwa sh.milioni 4 , pia wametoa sare na vifaa vya michezo vyenye thamani ya  shilingi milioni 1,150 pia  ukarabati wa shule ya msingi Ilendeja umegharimu Shilingi milioni 2,885.

Akiishukuru Kampuni hiyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Bukandwe Samiu Rugakingira amesema anaishukuru Kampuni ya Mbogo na anaomba Kampuni hiyo iendelee kuwa mlezi wa shule za msingi wa Bukandwe na  Ilendeja.

Naye mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi Bukandwe Jenifa Abuto aliyenufaika na ufadhili huo amesema Kampuni kama Mbogo ziendelee kuongezeka zaidi ili shule nyingi zaidi ziendelee kunufaika.

Akitoa salamu za Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Dkt. Philemon Sengati amesema Magu wanafanya mambo makubwa hawajawahi kumuangusha Mkuu wa Mkoa wa Mhe. John Mongella kwani hata uandikishwaji wa daftari la wapiga kura tumezidi asilimia tisini.

"Kata ya Bukandwe Mhe. Mkuu wa Mkoa  ni asilimia 20 tu kwenye umeme na maji, tunakuomba wataalamu wako waje watusaidie wananchi wa Bukandwe baba tushike mkono Bukandwe,"alisema Michael Minzi ambaye ni diwani wa kata ya Bukandwe.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.