UKAMILIFU WA HOTELI YA NSSSF MWANZA NI FURSA YA KUKUZA UCHUMI - RC MTANDA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Juni 11, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuwataka kuongeza nguvu katika ukamilishaji wa Hoteli ya NSSF inayojengwa Jijini Mwanza kwa kuwa uhitaji wa huduma za malazi bado ni mkubwa.
Mhe. Mtanda amesema Serikali imejikita katika miradi ya kufungua uchumi wa Kanda ya Ziwa, Aidha amesema Ujenzi wa Soko Kisasa la Mjini Kati litakwenda kuchagiza uchumi wa Wafanyabiashara na Wakazi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Sambamba na hilo, Mkuu wa Mkoa pia ameongeza Ukamilikaji wa Daraja la Kigongo - Busisi itarahisisha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo na itaokoa gharama ya muda ambapo Mwananchi anaweza kutoka Mkoani Geita akaja Mwanza kufanya manunuzi katika soko la mjini kati na akaweza kurudi Geita kuendelea na shughuli zake.
“Pia hapa Mwanza kuna ujenzi wa bandari ya kisasa ya north port, na Serikali pia imejenga meli kubwa ya mizigo na abiria ambapo tutaweza kwenda nchini Uganda kuchukua mizigo na kurudi Mwanza kwa wakati”.
Hivyo Mwanza imeunganishwa na ziwa ambapo tuna meli moya ya MV. Mwanza Hapa Kazi Tu, daraja la JPM, Reli ya kisasa ya mwendokasi na hivi tunavyoongea pia Serikali inafanya upanuzi wa uwanja wa ndege, Mwanza sasa itakuwa inafikika kwa njia zote hizo tatu. Ameongeza Mkuu wa Mkoa.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema ujenzi wa hoteli ya NSSF Mkoani Mwanza Bodi haijafanya makosa na amewataka kuendelea kuhakikisha hoteli hiyo inaenda kwa wakati, ukizingatia Mkoa wa Mwanza umekuwa na kawadia ya kupokea wageni wengi wa Kitaifa na Kimataifa hivyo ikienda kwa wakati na maendeleo hayo aliyoyataja hapo juu basi watakuwa wameweza kukamata soko la malazi.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Mwamini Malemi, amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa maneno na maelekezo yake mazuri na amesema bado wao kama Mfuko wa Hifadhi wataendelea kushirikiana kikamilifu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.