• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Viongozi wa Mwanza wapatiwa mafunzo uongozi wa uadilifu

Posted on: July 2nd, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amewaasa viongozi kuhakikisha kuwa katika kila jambo wanalolifanya waache alama ili wale wanaowaongoza waige mfano bora katika utendaji wao wa kila siku ikiwa ni pamoja na kuwa wabunifu na kufanya vitu tofauti ili kuleta maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Mhe.Mongella ameyasema hayo wakati akifungua semina ya viongozi ngazi ya Mkoa hadi Halmashauri inayofanyika katika Ukumbi wa  NIMR (MITU) kuanzia julai 2 hadi 4 ikijumuisha Waheshimiwa wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi,makatibu tawala wa Wilaya,waweka Hazina wa Halmashauri na baadhi ya Makatibu tawala wasaidizi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo na kuratibiwa na UONGOZI Institute kutoka Makao Mkuu Dar es Salaam.

"Kiongozi ni mfano, mtatuzi wa changamoto na mtoa mwelekeo wa  taasisi husika lazima aache alama,afanye vitu tofauti kwa maendeleo ya taasisi, jamii na Taifa kwa ujumla,alisema Mhe.Mongella.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa TAKUKURU  Dkt. Edward Hoseah akiwasilisha mada yake ya Uongozi wa Uadilifu amewaasa viongozi kuhakikisha wanasimamia,kulinda na kuangalia maslahi mapana ya Taifa na watu wengine na siyo maslahi yao wenyewe.

"Kiongozi muadilifu ni lazima awe mtu anayeamini katika haki na kufanya maamuzi magumu kwa kuzingatia taratibu sahihi na awe na ndoto na maono yanayotekelezeka,"alisema Dkt.Hoseah.

Dkt.Hoseah ameongeza kuwa hatuwezi kuwa na maendeleo kama hakuna viongozi waadilifu na kusisitiza kuwa ukiwa kiongozi muadilifu lazima kutakuwa na kitu kinachokupelekea kufanya jambo linavyotakiwa lifanyike kwani uadilifu huleta amani na mafanikio katika Taasisi,Jamii na Taifa zima.

Pamoja na kusisitiza maendeleo Dkt.Hoseah amezitaja mbinu za kupambana na rushwa  na kusema kuwa lazima kuwe na utashi wa kisiasa na uadilifu, mfumo imara wa uadilifu wa kitaifa pamoja na usawa, kwa maana kuwa waliopo  Serikalini hakuna anayependelewa. Vivyo hivyo  kuhusisha mfumo mzima kwa ukamilifu yaani Serikali isifanye kazi  peke yake.

Kwa upande wake Kaimu  Mtendaji Mkuu Taasisi ya UONGOZI Bw. Kadari Singo katika ukaribisho  alitumia muda huo kuwakumbusha viongozi umuhimu wa kufahamu na kufuata itifaki mbalimbali.Aidha alitoa mfano wa utoaji business card,ambapo alisema kiongozi wa ngazi ya chini haruhusiwi kumpatia business card kiongozi wa juu,ila pale tu anapoombwa kufanya hivyo.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Said Kitinga akachangia kuhusu namna mifumo na Sheria zilizopo Sasa zinavyojikita zaidi kumlenga mtu aliyepokea rushwa na kumwacha yule aliyetoa rushwa. Na kwamba Kama Taifa tutafakari ni jinsi gani tutaibadilisha mitazamo ya jamii ya kitanzania ambayo inamuona kiongozi aliyemaliza muda wake bila kujipatia utajiri,Kama mtu aliyeshindwa kunitumia nafasi yake vizuri. Hivyo kuihalalisha rushwa ndani ya jamii.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.