• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Visimbuzi vilivyofungiwa vyatolewa ufafanuzi

Posted on: October 9th, 2018


 Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) imekanusha kuipendelea television ya Taifa(TBC) kiliko chaneli nyingine zilizo hapa nchini.

Akitoa walisilisho kuhusiana na chaneli za maudhui yanayotakiwa yatolewe bila kulipia kwa viongozi na wadau mbalimbali mkoani Mwanza , Mkuu wa Kanda ya Ziwa TCRA Mhandisi Francis Mihayo alisema, si kweli kama malalamiko ya wananchi yanayosema t?TCRA inapendelea TBC.

“Baada ya kutoa maagizo ya kuzitoa zile chaneli kwenye vizimbuzi ambavyo haviruhusiwi ndipo yakaja malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba tunapendelea TBC sio kweli,hayo ni makubaliano ya kila nchi nenda nchi za Kenya au Uganda wanayo,kwahiyo kila nchi ilikubaliana chaneli ya taifa iliyopendekezwa na taifa husika lazima ibebwe kwenye visimbuzi vyote”alisema Mihayo.

Aliongeza kuwa,Tanzania kuna makampuni sita , visimbuzi vya star media, continental digiteki na kizimbuzi cha Tingi ni makampuni yaliyopewa dhamana ya kubeba chaneli tano za bure ambazo zilikuwepo wakati wa anolojia na cheneli zitakazozidi kwenye hizo tano zitaruhusiwa kulipiwa na yakaja makampuni ambayo ukitaka kuangalia chaneli yoyote lazima ulipe ambayo  ni dstv, zuku na azam.

“Kwa mujibu wa sheria ya shirika la mawasiliano duniani wakati tunakubaliana kutoka anolojia kwenda dijitali ilikubalika kwa kila nchi husika ni lazima ibebe zamana ya kurusha television ya taifa pasipo kulipisha kitu chochote ndipo mkanganyiko ulipotokea,”alisema Mihayo.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za jamii mkoani Mwanza, Hamidu Said alisema alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanajiuliza kwanini wanafungia vizimbuzi  na kusababisha wakose habari lakini baada ya kuhudhuria kikao cha TCRA ameelewa na kuwataka wanaopotosha waache maana wanaumiza vichwa vya watu.

Akiwakilisha waandishi wa habari mkoani mwanza, Albert Sengo alisema sheria zinazosimamia utendaji wa vyombo hivo,  hazina budi kufuatwa kadri miaka inavyosonga na zikionekana haziwapi manufaa wadau hao, hawana budi kurudi tena mezani na kuzijadili kwa ajili ya kuzifanyia marekebisho kuliko wamiliki hao kufanya maamuzi yao ambayo baadaye huwagarimu.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.