• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Wahandisi na Maafisa manunuzi watakiwa kutekeleza miradi ya ujenzi kwa kuzingatia Sheria,kanuni na miongozo

Posted on: April 5th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima amewataka wahandisi na maafisa manunuzi wa halmashauri kutekeleza miradi ya ujenzi kwa kuzingatia sheria ya usimamizi wa fedha za umma, manunuzi fedha za serikali  za mitaa na bajeti.

Agizo hilo la Mhe. Malima limetolewa Mei 4, 2023 jijini hapa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi  kwa niaba yake alipokuwa akisoma hotuba  ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wahandisi wa mikoa na halmashauri pamoja na maafisa manunuzi kuhusu usimamizi wa ujenzi wa miundombinu ya shule za elimu ya awali na msingi kupitia mradi wa BOOST.

“Ili kupata thamani ya fedha na kuepuka hoja za ukaguzi mnapotekeleza miradi ya ujenzi zingatieni sheria, kanuni na miongozo, kama mnavyojua mradi wa BOOST ni lipa kwa matokeo sasa ili mradi huo uweze kufanikiwa na kuwa na tija tunawategemea sana nyie kufanya  kazi kwa weledi, mkizingatia taratibu na maelekezo yote na kutimiza masharti na vigeo vya uhakiki vitakavyotumiwa na Wakala Huru wa Uhakiki”amesema Mhe. Makilagi.

Mhe. Makilagi ameongeza kuwa serikali inatarajia kujenga jumla ya vyumba 12,000 vya madarasa katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa mradi wa BOOST kwa kuanzia mwaka wa pili wa utekelezaji wa mradi  huo wastani wa vyumba 3,000 vitajengwa.

“Nyie tunawategemea sana katika kutekeleza miradi nawasihi msibadilishe maeneo ambayo yatapangwa kujengwa shule au ukarabati wa miundombinu maana Ofisi ya Rais TAMISEMI ilishafanya tathmini ya ujenzi wa shule na ukarabati wa mindombinu chakavu maeneo yatakayopewa kipaumbele ni yenye msongamano mkubwa wa wanafunzi, vijiji vyenye ukosefu wa shule, maeneo ambayo wanafunzi wanatembea umbali mrefu na shule za msingi  zilizobainika kuwa na uchakavu mkubwa,”amefafanua Mhe. Makilagi na kuongeza

 “Endapo kuna uhitaji huo halmashauri inapaswa kuwasilisha maombi hayo kwa Katibu Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia kwa Katibu Tawala wa mkoa ili kupata idhini hiyo,”ameeleza Mhe. Makilagi.  

Aidha Mhe. Makilagi amempongeza Rais  Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za dhati katika kuondoa kero za ufundishaji na ujifunzaji shuleni ambapo ametoa fedha zaidi ya Sh bilioni 230 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule 1,338 za msingi zilizopo katika mikoa na halmashauri zote nchini .

“Rai yangu kwenu washiriki wa mafunzo haya imarisheni  ushirikiano ngazi ya halmashauri pia tekelezeni  ujenzi wa miundombinu kwa wakati na kwa ubora mkisimamia ujenzi wa miundombinu hiyo kwa  weledi na uadilifu pia epukeni migogoro ambayo huchangia kucheleweshwa utekelezaji wa miradi,” Mhe. Makilagi amewaasa wahandisi hao pamoja na maafisa manunuzi.

Awali  Mratibu wa Mradi wa BOOST OR- TAMISEMI, Joel Mhoja  alimwambia  Mhe. Makilagi kwamba mafunzo hayo yamewakutanisha washiriki 192 kutoka mikoa mbalimbali nchini  lengo likiwa ni kuwajengea uwezo  ili wawe na nafasi ya kusimamia vizuri utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu kupitia mradi huo.

“Washiriki  wa mafunzo haya yaliyofanyika kwa siku mbili mkoani hapa wamejengewa  uwezo juu ya ramani za mpangilio wa majengo na mapitio yake, utambulisho wa DLI na vigezo vya uhakiki, usalama wa mazingira, tafsiri rasmi ya taratibu za manunuzi na utunzaji wa kumbukumbu za manunuzi,”alisema Mhoja.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.