• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Wakaguzi wa Mazingira Wakabidhiwa Majukumu

Posted on: May 30th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema  Mhe.Emmanuel Kipole  kwa niaba ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ametoa vitambulisho 23 kwa wakaguzi wa Mazingira kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  wa Mwanza.

Vitambulisho hivyo vimetolewa kufuatia kifungu cha 183(2) cha Sheria ya usimamizi wa Mazingira,Baraza  la Usimamizi  wa Mazingira  Makao Makuu lilitengeneza vitambulisho 23 kwa ajili ya maafisa walioshiriki mafunzo ya wakaguzi wa Mazingira, ambapo walengwa wamekabidhiwa vitambulisho hivyo ili waweze kushiriki kwa ukamilifu kwenye usimamizi na  ufuatiliaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya Plastiki.

"Zoezi hili ni la kishwria kama Mkoa hatutaki kusikia linafanyika tofauti na Mikoa mingine maana maelekezo ni yaleyale na yametolewa na mtu mmoja ambaye ni Makamu wa Rais kila mmoja afuate sheria.

"Anayestahili kupigwa faini apigwe kiharali bila kuaangalia chwo wala kiwango cha fedha alizonazo, kazi hii isiwe ya rushwa naombeni mkafanye kazi kwa uwazi, " alisema Mhe Kipole.

Pamoja na kukabidhiwa vitambulisho hivyo,moja ya mamlaka waliyopewa ni kuingia kwenye jengo lolote,ndani ya ndege, chombo cha majini,ardhini au sehemu yoyote isiyo na makazi ya watu.

Pia kusimamisha chombo chochote na kufanya ukaguzi,kuchukua sampuli,kupiga picha,kukamata chombo na kutoa agizo kwa mujibu wa sheria.

Akiongea katika makabidhiano hayo Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Christopher Kadio amesema tarehe 12 hadi 14 desemba 2018 Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira  lilifanya mafunzo  kwa wakaguzi 23 wa Mkoa wa Mwanza.

"Lengo ilikuwa ni kuwajengea uwezo wa kufanya ukaguzi wa mazingira pamoja na kuwakumbusha  maadili wakati wa utekelezaji wa majukumu ya  Wakaguzi wa Mazingira  kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na.20 ya Mwaka 2004, alisema Kadio".

Aidha, Kadio ameongeza kuwa wateuliwa wamekidhi sifa za kuwa Wakaguzi wa Mazingira zilizoelekezwa na Ofisi ya  Makamu wa  Rais ambazo ni uadilifu wa Mtumishi na asiwe na taarifa  za Uhalifu, awe na uchapakazi na  ushirikiano, awe mtumishi yeyote wa Umma na awe na Taaluma yoyote inayohusiana na Shughuli za Mazingira.

Hata hivyo Mmoja kati ya wakaguzi waliopata vitambulisho hivyo kutoka Wilaya ya Magu Ngusa Buyamba amesema dhamana waliyopewa ni kubwa hivyo wataitendea haki ili kuepuka kutokuelewana kwa Serikali na wananchi.

"Ahadi yetu ni uadilifu majukumu tuliyopewa ni makubwa naombeni uamuzi wa mwisho uhusishe mwajili wako," alisema Buyamba.

Kwa upande wake Afisa Misitu na Mratibu wa Shughuli za Mazingira Mkoa wa Mwanza Mangabe Mnilago amesema Serikali imewaamini na kuwapa mafunzo hivyo watahakikisha wanatenda haki na kutimiza wajibu wao ili mazingira yawe salama kila mmoja atimize azma ya Serikali ya kutunza mazingira.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.