• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

WANAHABARI MWANZA WATAKIWA KUTOA HABARI SAHIHI KUELIMISHA JAMII

Posted on: December 14th, 2024

WANAHABARI MWANZA WATAKIWA KUTOA HABARI SAHIHI KUELIMISHA JAMII


Waandishi wa Habari mkoani Mwanza wamekumbushwa kuzingatia maadili ya taaluma yao wakati wanatimiza majukumu ya kila siku ili jamii ijengwe kwenye misingi ya ukweli.

Rai hiyo imetolewa jana tarehe 13 desemba, 2024 na mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubiagai kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye hafla ya usiku wa Wanahabari iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mwanza Hoteli.

Amebainisha vyombo vya habari ni muhimili muhimu hivyo ili kuepuka migongano isiyo na tija waandishi wa habari wana wajibu wa kujiridhisha na usahihi wa kile wanachokusudia kuwafahamisha wananchi.

"Ndugu zangu wana habari wote hapa ni mashuhuda Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anavyozidi kuwawekea mazingira mazuri ya kazi zenu na hasa anavyosisitiza ushirikiano baina ya Serikali na vyombo vya habari, tuendelee kutumia kalamu zetu vizuri na hata pale kwenye kukosoa  uungwana utumike na isiwe karaha kwa mlengwa,"mkuu wa wilaya.

Comrade Ngubiagai ametolea mfano Mkoa wa Mwanza umekuwa na miradi mingi ya kimkakati,waandishi wa habari wanatakiwa kutumia nafasi hiyo ili wananchi wapate ufahamu wa kina namna Serikali yao inavyowaletea maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha waandishi habari mkoani Mwanza,MPC Bw.Edwin Nsoko amesema huo ni utaratibu waliojiwekea wa kila mwaka kuwa na usiku wa pamoja kwa kushirikiana na wadau wao mbalimbali na kubadilishana uzoefu wa shughuli zao.

"Mheshimiwa mgeni rasmi kazi zetu zinahitaji ushirikiano wa dhati ili kutimiza vizuri majukumu yetu hapa zipo Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ambazo tumeshirikiano nazo kuhakikisha tunajenga uchumi wa Taifa letu,"Mwenyekiti MPC

"Hivi sasa tunazidi kujiimarisha katika sekta ya usafiri wa maji kwenye maziwa ya Victoria,Tanganyika na Nyasa,Meli mpya  ya Mv Mwanza ipo mbioni kuanza safari zake na itafika hadi Kenya na Uganda,ni dhahiri shughuli za kiuchumi zitapiga hatua hivyo vyombo vya habari vina wajibu wa kuwaemisha wananchi fursa zilizopo kupitia mradi huu,"Erick Hamisi,mkurugenzi mtendaji TASHICO.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.