• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Wananchi Magu wapongezwa kwa kampeni ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa

Posted on: July 26th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel anaendelea na Kampeni ya Ujenzi wa Miundombinu ya Madarasa ambapo leo ameungana na maelfu ya wananchi na wadau kuchimba Msingi wa Madarasa 44 katika shule ya Msingi Bujora wilayani Magu.

Akizungumza na wananchi hao walioshiriki uchimbaji wa Msingi kwenye shule hiyo amewapongeza kwa kuonesha kiu ya kujiletea maendeleo na amebainisha  kwa kujitolea huko ni dhahiri wanamuunga mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa vitendo.

"Maendeleo ya wananchi wa Mwanza yataletwa na wanaMwanza wenyewe, hongereni na Mungu awabariki sana kwa jambo hili kubwa mlilofanya na msiache tabia hii njema kwani desturi ya kutoa inatupa heshma sana na hadhi hata mbele za Mungu kwani kutoa ni moyo na sio kwa sababu ya kuwa unavyo vingi bali ni kwa upendo kwa watoto wetu." Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Salum Kali amewashukuru wananchi waliojitokeza kwa hamasa kubwa kuchangia nguvu kazi kwenye kampeni ya Ujenzi wa Madarasa na ametumia wasaa huo kuwakumbusha kujiandaa kushiriki zoezi la Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022.

"Namshkuru sana ndugu yetu Mkuu wa Mkoa kwa kazi anayofanya akishirikiana na viongozi wenzake nasema mnakitendea haki Chama Cha Mapinduzi kupitia Ilani, sisi kama wasimamizi tunaridhishwa na Maendeleo haya." Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Magu.

"Nimetoa matofali 400 kwa ajili ya watoto wetu nawaomba tumuunge mkono Mhe. Rais Mama Samia kwani anatujali sana wananchi wa Mkoa wa Mwanza na ndio maana mnaona anatufanyia mengi kwenye kila sekta." Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Mhe. Kabula Shitobelo.

"Hapa vinahitajika vyumba 44 na watoto hawa ni wetu wote  ila hata mwalimu akiwa na uwezo namna gani hawezi kufundisha wanafunzi 175 ndani ya darasa moja hivyo tuendelee kuchangia nguvu kazi, nami pamoja na matofali ya Mhe Mbunge wa viti Maalum nitahakikisha yanaletwa matofali 2000 hapa leo hii." Mhe. Kiswaga Deus, Mbunge Magu.

"Wanabujora mmepata bahati kiwilaya, Mhe Mkuu wa Mkoa tunakushuruku sana tunahitaji viongozi kama ninyi ambao mnatambua changamoto za wananchi wa chini na kuwasaidia, sisi kama Halmashauri tunapeleka fedha kwenye miradi hii kwa ajili yakuikamilisha." Mhe. Simon Mpandalume, Mwenyekiti Halmashauri ya Magu.

"Mimi kama mwenyekiti wa Kitongoji hiki natoa matofali 800 kwenye Ujenzi huu maana nilifurahishwa sana niliposikia kuwa Mkuu wa Mkoa atakuja hapa kuanzisha ujenzi wa Madarasa na nilisema kwakweli ni jambo jema na sitamuangusha," amesema Mhe. Doto Mtimkavu.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.