• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Wananchi wa Igalula waanza kulipwa fidia kupisha shughuli za Mgodi

Posted on: September 4th, 2023

Wananchi wa Igalula waanza kulipwa fidia kupisha shughuli za Mgodi


Zaidi ya Shilingi Bilioni 60 zinatarajiwa kulipwa kwa wanufaika 853 kwenye Vijiji vya Sotta na Nyabila kata ya Igalula- Sengerema ili kupisha shughuli za uchimbaji Madini ya Dhahabu Nyanzaga Mgodi unaomilikiwa kwa Ubia Kati ya Kampuni ya Ore Corp Limited (84%) na Serikali ya Tanzania (16%).

Akizungumza leo Septemba 04, 2023 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi akiwa kwenye hafla ya kukabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 3.7 ambazo zimeshalipwa kwa waguswa ikiwa ni ishara ya kuendelea kwa zoezi la ulipaji fidia kwa wanaopisha shughuli za uchimbaji ameipongeza kampuni hiyo.

Amesema, waguswa 152 sawa na asilimia 17.8 ya ambao hawajasaini mikataba ya fidia wanapaswa kufanya hivyo na kujiandaa kupisha kwenye maeneo na hata wanaojengewa nyumba kufanya hivyo mara tu watakapopata nyumba zao na kwamba serikali ipo bega kwa bega kusimamia haki za wananchi na mwekezaji kwa manufaa ya Taifa.

Mhe. Makilagi amesema hatua iliyofikiwa na ulipaji wa Fidia kwa wananchi ni ishara njema ya kuanza rasmi kwa shughuli za uchimbaji kwenye eneo hilo hivyo ni wajibu wa wanufaika walichangamkie na akatoa wito kwa wananchi wa Sengerema kujiandaa na fursa za kiuchumi kama ajira na kufanya biashara kutokana na uwepo wa Mgodi huo uliowekeza zaidi ya Trilioni 1.

Vilevile, ametumia wasaa huo kumpongeza Rais Samia kwa uongozi imara uliopelekea ongezeko la Pato la Taifa kwenye sekta ya madini hadi kufikia Asilimia 10 kutokana na makusanyo makubwa na kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi ya kimkakati ambayo  inaleta si tu uboreshaji wa huduma za jamii bali ukuaji wa uchumi wa nchi.

Hata hivyo, ametoa wito kwa kampuni hiyo na makampuni mengine Madogo yaliyoingia mkataba na kampuni mama kuhakikisha wanatekeleza vema sheria ya kurejesha faida kwa jamii inayozunguka na ushuru wa huduma kwa kulipa kodi zote stahiki kwa serikali kuu kupitia Mamlaka ya mapato nchini (TRA) na ile ya halmashauri.

"Kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu kumekua na mabadiliko ya Tabia nchi hivyo natoa wito kutochafua vyanzo vya maji na kuhakikisha mnatunza mazingira na kuhakikisha mnalilinda ziwa letu na mjiepushe na ukataji wa miti ili kuepusha athari za kimazingira na wananchi naomba tujenge tabia ya kupanda miti" Mhe. Makilagi.

Akizungumzia utekeleaji wa mpango wa uhamishaji watu na makazi, msimamizi wa miradi ya kampuni hiyo nchini Isaac Lupokela amesema hadi Septemba 02, 2023 waguswa 701 wameshapata ufafanuzi wa stahiki zao na wamekwisha saini mikataba na kwamba mikataba 190 imekamilika na kuchukuliwa na waguswa na uelimishaji unaendelea.

"Tunaendelea na kazi ya Ujenzi na utaajiri maelfu ya watanzania wa maeneo ya jirani ambapo tunatarajia kuwaajiri zaidi ya watu elfu moja  na zitakuwepo pia ajira za muda, zoezi la uchimbaji dhahabu litakua na manufaa kwa Sengerema na Taifa kwa ujumla, na fedha za ulipaji fidia tayari zipo kwenye akaunti." Amefafanua bwana Lupokela.

Amefafanua kuwa leseni namba 653 ya mwaka 2021 iliwapa kampuni hiyo eneo lenye ukubwa wa Hekta za Mraba 23. 4 na kwamba kwakua kulikua na Kaya zinazoishi ndani ya eneo hilo walipashwa kufanya uthaminishaji  ili kulipa fidia stahiki kabla ya kutwaa ardhi hiyo kwa mujibu wa sheria jambo ambalo linafika mwisho siku za usoni.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.