• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Washonaji wa barakoa waaswa kufuata maelekezo kukidhi vigezo

Posted on: May 14th, 2020

Waziri wa viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa (Mb)amefanya ziara ya kikazi Mkoani Mwanza lengo ikiwa ni kufuatilia maendeleo ya Sekta ya Viwanda,ambapo ametembelea  kiwanda kidogo cha kutengeneza barakoa  cha Felister na kushuhudia shughuli za uzalishaji zikiendelea kiwandani hapo.

Akiwa katika kiwanda kidogo cha Feliste Mhe. Bashungwa amesema anatembelea ili kutoa uhamasishaji kwa washonaji wote nchini hususani wa vyerehani   kwa ngazi zote kuendelea kushona barakoa huku wakifuata maelekezo ya Mamlaka ya dawa  na vifaa tiba(TMDA) pamoja na TBS ili kushona barakoa zenye viwango vinavyo kubalika nchini.

"Naelekeza TBS na TMDA kwenda kwenye vyombo vya habari,kwenda mikoani na kutoa elimu kwa washonaji wa ngazi zote kuendelea kushona barakoa kwa ajili ya kuwapatia watanzania maeneo yote hata vijijini ziweze kupatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu," alisema  Mhe.Bashungwa.

Aidha amesisitiza kuwa amefika kwa mzalishaji mdogo ili kuonyesha mfano kuwa si lazima kiwe kiwanda kikubwa ndiyo lizalishe barakoa kwani hata kata na kijiji mmoja mmoja anaweza kutengeneza kwani kuna wanakijji pale kijijini wanaozihitaji kwa bei nafuu na kwa urahisi..

Kwa upande wa Mkurugenzi wa kiwanda hicho bi Felista Matoke Nyangwe amesema  tumeona fursa ya kuchangia katika jamii katika kipindi hiki kigumu cha ugonjwa wa corona (Covod -19) na tukaanza uzalishaji wa vifaa tiba tajwa tangu mwezi machi na tumekuwa tukipeleka TMDA  ili wathibitishe ubora wake kwa kufuata maelekezo waliyotupatia.

"Kwa sasa tunaweza kutengeneza barakoa pcs 35,000 kwa siku na tunayo ziada ya pcs 70,000 ndani,tunaweza kutengeneza coverall suit pcs 500 kwa siku  pia faceshields 70,000 kwa siku moja," alisema Nyangwe.

Alisisitiza kuwa kwa barakoa wanazotengeneza unaweza kufua na kuzinyooshe pia  changamoto iliyokuwepo ilitatuliwa na mganga mkuu mara baada ya kuwatembelea aliwapa ushauri wa material za kutumia na mashine ambazo zitawasaidia kurahisisha utengenezaji wake.

Nao watengenezaji wa barakoa wa kampuni ya Ushinaji ya Diva Vitenge  Khadija Liganga amesema wanatengeneza barakoa za aina zote hadi za watoto na wamepata mafunzo maalum kutoka TMDA na wanafuata ubora ulioelekezwa.

"Tunatengeneza size mbalimbali hadi za watoto na tunaamini pia Serikali yetu inaongozwa na chama cha mapinduzi hivyo tumefanya special kwa ajili ya chama cha mapinduzi kama mliiona hii ilisambaa sana kwa waheshimiwa ni sisi tulitengeneza,"alisema Liganga.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.