• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Watanzania msifurahie kuzaa na kusahau kulea watoto - DPP

Posted on: July 18th, 2019

Mkurugenzi wa Mashitaka  nchini (DPP), Biswalo Mganga amewataka watanzania  wasifurahie kuzaa  bali wanapaswa kutambua  kulea na kumtunza  mtoto katika maadili mema ni jukumu la wazazi na si vinginevyo.

Kauli hiyo aliitoa  jijini Mwaza  katika ziara yake ya kuendelea kutembelea magereza mbalimbali na kuzungumza na wafungwa na mahabusu  ambapo alisema  ameshuhudia watoto chini ya miaka 18 akiwa katika magereza lakini wengi wao wakiwa na kesi ndogo ndogo.

“Jamani tukumbuke watanzania tunakadiriwa kufikia milioni 55, kwa hiyo msongamano wa watu magerezani  unatokana na ongezeko la watu  lakini jambo ambalo nimeliona kule hasa kwa upande wa watoto, wengi wao wapo kule kutokana na kukosa malezi mazuri  na msaada kutoka kwenye familia zao.

 Mganga ambaye jana alikuwa katika Wilaya ya Sengerema na Ukerewe,  aliwataka mahakimu na polisi kuangalia kesi ambazo zinaweza kumalizwa kwa  mazungumzo ya kuwashauri  au kuwapa adhabu mbadala bila kuwapeleka magarezani.

Kwa upande wa Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Balozi Dkt. Agustino Mahiga alisema baada ya ziara hiyo ya kutembelea mikoa yote atakwenda kuzifanyia kazi changamoto zote atakazokutana nazo zikiwamo upungufu wa mahakama ambapo aliahidi kwamba lengo la Serikali ni kuona kila wilaya inakuwa na mahakama ya mwanzo naya wilaya.

“Kama mnakumbuka Mhe.Rais Dkt. John Magufuli alifanya mabadiliko na mimi nikaletwa katika wizara hii hivyo bado ni mgeni, ziara hii inakuwa na mambo mengi likiwamo kujitambulisha na kuona  kwa uhalisia changamoto zilizopo ambazo hata wabunge wamekuwa wakizisema bungeni.

“Jambo ambalo mpaka sasa nimeliona ni ratio (kiwango) cha watu waliopo magerezani ni kukibwa kuliko uwezo wake, yaani kila palipo na mfungwa mmoja kuna mahabusu wanne, sasa kwanza nitaanza kuhakikisha mahakama za mwanzo na wilaya zinajengwa, pia tutaangalia idadi ya watumishi,”alisema.

DPP Mganga aliwachia huru wafungwa  na mahabusu 325 katika magereza  mbalimbali Kanda ya Ziwa wakiwamo askari nane  wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakituhumiwa  na kesi ya  uhujumu uchumi namba 1/2019 ya dhahabu yenye  uzito wa kilo 323.6 na fedha taslimu Sh. milioni 305.

Katika gereza la Butimba jijini Mwanza aliwaachia huru wafungwa na mahabusu 75,  Shinyanga  25, Kahama 43, Mugumu 52, Bunda 24, Bariadi 100 na Tarime 6.

Alisema  sababu  zilizofanya kuachiliwa kwa mahabusu na wafungwa hao ni  kubambikiwa kesi, ugonjwa, umri na tuhuma nyingine zenye harufu ya rushwa kuanzia kwa raia wenyewe kwa wenyewe, mpelelezi hadi kwa hakimu.



Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.