• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Watoto waishio Mitaani,wafanyakazi wa majumbani kupatiwa Elimu ya haki zao

Posted on: April 22nd, 2021

Maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii , Polisi ,Raiway Children Africa ,WoteSawa na mashirika yasiyo ya serikali wametakiwa kushirikiana na serikali kutoa elimu ya haki za watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani na wafanyakazi wa nyumbani.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza  Emmily Kasagala wakati wa utambulisho wa mradi mpya wa kuwezesha upatikanaji wa haki za wafanyakazi wa nyumbani na watoto na vijana wanaoishi na kufanyakazi mitaani kupitia kutoa elimu ya sheria katika Wilaya ya Ilemela na Nyamagana.

Alisema ushirikiano huo utasaidia kutatua matatizo ya watoto wa makundi hayo na kuzuia ongezeko la kuja mitaani na kupunguza unyanyasaji wa wafanyakazi wa majumbani hivyo kila mmoja aone anao wajibu wa kumlea na kumwongoza mtoto ili afikie malengo yake ya badaye.

Alisema suala la watoto wadogo kushinda mitaani , unyanyasaji wa wafanyakazi wa nyumbani ,usafirishaji haramu wa watoto siyo sahihi kutokana na haki wanazostahili kupata kwa kujibu wa sheria ya mtoto hivyo wakati umefika wa kukabiliana na sababu zinazochangia watoto kukaa mitaani,kunyanyaswa na usafirishaji haramu .


Alisema ndani ya mwaka mmoja  Railway Children Africa na Wotesawa wamewaokoa watoto 353, ambapo wamewarejesha nyumbani watoto wapatao 193 na wamefanikiwa kutoa msaada wa kisheria kwa watu 274 na kutoa mafunzo na kuwawezesha kiuchumi familia na vijana 189 huku wakiwaunganisha shule na mafunzo mbalimbali ya ufundi watoto 316.


" Tunatambua zipo sababu nyingi zinachangia adha hii ni vitendo vya ukatili ngazi za familia,vitendo vya ukatili mashuleni,ugomvi miongoni mwa wazazi au walezi,kuachana kwa wazazi,hali duni ya uchumi wa familia ,waajiri wa wafanyakazi kutokuwa waadilifu, ukosefu wa elimu ya sheria ya mtoto,kutofanya Kazi kwa kamati za ulinzi wa mtoto ngazi ya kata na vijiji na changamoto za makundi rika naimani na huu mradi mpya utaleta nuru " alieleza Kasagala


Alisema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali katika kuchangia katika mpango wa taifa wa ulinzi wa watoto kwa mwaka 2017/ 2018  na 2021 hadi 2022 japokuwa takwimu za watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani na wanaofanya kazi za nyumbani katika Mkoa wa Mwanza zinaonekana kukua na kuongezeka kadri siku zinavyokwenda .

Alisema kutokana na zilizopatikana hivi karibuni kutokana na zoezi lililoendeshwa kati ya shirika Railway Children Africa kwa kushirikiana na PACT Tanzania na Cheka sana Tanzania pamoja na serikali kupitia Halmashauri za Ilemela na Jiji la Mwanza zinaonyesha kuna watoto 1254 waliohesabiwa mitaani ambapo watoto 978 (78%) , waliohesabiwa nyakati za mchana  na 276 (22%) nyakati za usiku.

Aliongeza kuwa kupitia utafiti uliofanyika mwaka 2020 wa kumlinda mtoto nchini kwa kutathmini kuongeza wigo na matokeo ya matumizi ya sheria ndogo zinazomlinda mfanyakazi wa nyumbani unaonyesha manispaa ya Ilemela na Nyamagana kuna wafanyakazi wa nyumbani 6,286 .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la WoteSawa ambaye pia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Raiway Children Africa Angela Binedcto alisema wanatamani kuona jamii ambayo ni salama ,huru na uwazi pamoja na uwepo wa mfumo wa sheria ambayo itaonyesha wafanyakazi wa nyumbani wanafanya kazi katika mazingira salama.

Alisema watoto hao wanakabiliana na matatizo mengi ikiwemo ukatili wa kingono na malipo yasiyoendana na utendaji Kazi wao hivyo kupitia mradi huo WoteSawa na Raiway Children Africa wataimarisha kukuza mifumo ya utoaji  haki na msaada wa kisheria kwa wafanyakazi wa nyumbani , watoto na vijana wanaoishi na kufunya Kazi mtaani.

Aliongeza kuwa wataongeza kuelewa na ujuzi kwa jamii kuhusu ulinzi wa haki za watoto huku matarajio yao yakiwa ni kuongezeka upatikanaji wa msaada wa kisheria na saikolojia kwa makundi hayo pia mradi huo utafanya kazi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kirumba, Buhongwa,Igoma,Kayenze,Luchelele,Kitangiri , Bugarika ,Mkuyuni Buswelu ,Machina,Igogo , Mabatini na Bugongwa.


Naye Kaimu Meneja wa Shirika la Railway Children Africa Mkoa wa Mwanza Mary Mushi alisema kwa kipindi cha mwaka  mmoja 2020 wameweza kuoka kutoka mtaani watoto wapya 291,walitoa huduma za afya kwa watoto 240, huduma ya chakula kwa familia  91,kusaidiwa kuanganishwa na shule na kupewa vifaa watoto 301,kuwapeleka vijana 83 katika vyuo vya elimu ya ufundi, ,waliowezesha vijana 57 kufanya ujasiliamali,waliwaunganisha na kuwarejesha watoto143  na familia zao huku familia 72 ziliwezeshwa kibiashara.

Alisema mradi huo mpya utawapa wigo na kufanya kazi na jamii zaidi na kuleta chachu  itakayosaidia kuondokana matatizo hayo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.