• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

"Watumishi Tatueni kero za wananchi" - Mongella

Posted on: June 9th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongella, amewaonya na kuwataka watumishi wa Mkoa huo kufanya kazi pamoja na kutatua kero za wananchi.

Mhe Mongolla aliitoa  onyo hilo katika kikao cha upokeaji  taarifa ya utekelezaji wa  zoezi la  uanzishwaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi  Tanzania (HPV) kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 mkoa wa Mwanza.W

Mhe Mongella alisema, Kila mtumishi akifanya kazi bila visingizio, kuwajibika kwa nafasi yake na kutekeleza mipango na maelezo ya Serikali, suala la wananchi kujitokeza na mabango ya malalamiko kwa viongozi wa Kitaifa litapungua.

“Sipendezwi na mabango ya wananchi yanayoonesha awatatuliwi kero zao, na yeyote atakayezembea kuwahudumia wananchi kwa nafasi yake na malalamiko yakajitokeza kwa viongozi wa Kitaifa atawajibishwa”,alisema Mhe Mongelle

Aliongeza pia, wapo baadhi ya watumishi wanakwamisha mipango ya Serikali kutokana na tabia yao ya kuwa na  visingizio vingi, kutaka wabembelezwe  kutimiza wajibu wao na kuwataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mkoa wa Mwanza kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi kila baada ya miezi mitatu.

 “Twendeni vijijini tukawahudumie wananchi, mfano katika hili la saratani linakwamisha sana maendeleo kwani mama mmoja akiwa na saratani lazima familia itayumba hata kama wana uwezo wa fedha, tambueni asilimia 80 ya shughuli za nyumbani zinafanywa na mama,bila kusimamia afya na uhai wa watu tutakuwa tunajidanganya kupata maendeleo”alisema

Naye Afisa wa Mpango wa Taifa, Kitengo cha chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi  Tanzania (HPV)  kutoka wizara ya afya, Pricilla Kinyunyi alisema kwa mujibu wa takwimu kutoka  Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha jumla ya watanzania 50,000 wanapata maambukizi mapya na asilimia 70 ya wagonjwa hao wanajitambua wakiwa katika hatua ya nne ambayo ni hatari.

Alisema asilimia 36 ya wagonjwa hao waliogundulika na saratani  wanapoteza maisha, hivyo aliwashauri wazazi kuwatunza mabinti wao na kuwashauri kuepuka  kuanza ngono mapema sambamba na  kuwahimiza kupata chanjo wanapofikisha umri wa miaka 14.



Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.