• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Watumishi wanne Jiji la Mwanza wasimamishwa kazi kwa utovu wa nidhamu

Posted on: January 13th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima amemuagiza Katibu Tawala Mkoa huo kuwasimamisha kazi kwa Siku Saba Mkuu wa Idara ya Ardhi Robert Phales, Ayubu Kasuka Halima Nassor na Yuster Zephrine kuanzia leo Januari 13, 2023 ili kupisha uchunguzi kutokana na utovu wa nidhamu.

Mhe. Malima ameongeza kuwa Ofisi yake imeandika Barua TAMISEMl ya kuomba achukuliwe hatua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndugu Sekiete Yahya kwa kukiuka Maelekezo ya Kamati ya Usalama Wilaya ya Tarehe 28, 09, 2022 yaliyozuia uuzwaji wa Viwanja Namba 194 na 195 vilivyopo kwenye mtaa wa Rwegasore na wao kuamua kuviuza kwa Milioni 500 kila kimoja.

"Tumemkuta Mkurugenzi wa Jiji na Makosa makubwa sana ya kukiuka maelekezo ya Kamati ya Usalama Wilaya na ameonesha aheshimu kabisa Mamlaka zilizo juu yake kwa utovu huo wa nidhamu alioufanya ambapo alitengeneza hoja ya kuuza viwanja hivyo isivyo halali na tumebaini kuwa endapo vingeuzwa kwa njia ya Mnada basi vingeuzwa kwa zaidi ya Milioni 500 kila kimoja."

Katika hatua ingine, Malima amesema Ofisi yake imeunda Kamati ya kuchunguza Sakata hilo kwa siku Saba itakayoongozwa na Mkurugenzi wa Maadili wa Kanda ya ziwa Ndugu Godson Kweka huku ikihusisha wataalamu kutoka Ofisi za  TAKUKURU, Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa pamoja na Ofisi ya Mashtaka (DPP).

"Terehe 28, 9, 2022 Kamati ya Usalama Wilaya iliitaka Halmashauri ya Wilaya ya Jiji isiviuze viwanja namba 191 hadi 195 vilivyopo kwenye mtaa wa Rwegoshora bila ya idhini ya Kamati hiyo lakini wao wakaamua kuviuza kwa Tshs Bilioni Moja." Malima amefafanua.

Amefafanua kuwa, awali Kamati ya Usalama Mkoa imefanya uchunguzi na kubaini kuwa viwanja hivyo vimeuzwa kinyemela bila kumtaarifu Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Halmashauri imekiri kuviuza na kusema wamefanya hivyo kwa ruhusa ya Ofisi ya Rais Ikulu, TAMISEMl na Wizara ya Ardhi jambo ambalo si kweli.

"Viwanja  hivi haviruhusiwi kuuzwa, kufanyiwa Ujenzi wala kuendelezwa kwa namna yoyote mpaka pale suala hili litapomalizika na endapo itaonekana wamiliki wanastahili kuendelea watapata taarifa na kwa upande wa Halmashauri nnaagiza fedha zilizopatikana kwenye uuzwaji wa viwanja hivyo zisitumike ili itapobainika kumekua na ukiukwaji wa uuzwaji basi wamiliki watarejeshewa fedha zao." Mhe. Malima.

Katika hatua ingine Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imetoa Onyo kali kwa Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Watumishi wa Idara ya Fedha na Uhasibu, Afisa Manunuzi, Mwanasheria na Mkaguzi wa Ndani kujitathmini kwenye Utendaji wao kwani wameonekana kutosaidia Halmashauri ipasavyo na itatoa Onyo kali kupitia Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa.

"Mwanza haiwezi kuwa kichwa cha Mwendawazimu kwamba kila mmoja anakuja kupiga pesa, kama watu wameingia kufanya tamaa na kuhusika na suala hili basi kwa dhamira yetu kama Viongozi wa Mkoa tutakwenda kutoa mfano kwenye suala hili kwa kutoa adhabu kali." Mkuu wa Mkoa.

Halikadhalika, Mkuu wa Mkoa ameiagiza Halmashauri ya Jiji kuboresha Mazingira Rasmi ya wafanyabiashara wadogo (Machinga) ili wafanye biashara kwa utulivu na kukomesha tabia ya kufanya biashara kiholela kwenye mji huo hali inayochafua taswira ya Mkoa huo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.