• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Waziri Mkuu afungua Kikao ALAT Mwanza

Posted on: July 23rd, 2019


Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa wamewaagiza wakurugenzi wote nchini  kufanya tathmini kwa kila halmashauri kwa kupitia ahadi zote za Rais Mhe.Dkt. John Magufuli alizozitoa wakati akiomba kura na kuainisha  katika makundi matatu iliziweze kutekelezwa kabla ya kurudi kwa wananchi kuomba ridhaa nyingine.

Aliekeleza kuwa   ahadi  ziwekwe katika mpangilio wa zilizotekelezwa, ambazo zimeanza kutekelezwa na zile ambazo hazijatekelezwa kabisa na kila kundi liainishwe  kilichokwamisha au changamoto iliyopo.

Agizo hilo amelitoa jijini Mwanza wakati  akifungua mkutano wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT)  ambapo  alielekeza  baada ya taarifa ya  tathmini hizo kukamilika zinapaswa kutumwa  kwake  ili Mhe.Rais Magufuli aweze kuzitimiza kabla ya kurejea kwa wananchi kuomba ridhaa kipindi cha pili.

“Rais wetu Mhe. Dkt. Magufuli anafanya kazi kubwa kweli kweli, ikumbukwe mwaka huu ni wa nne tangu ameingia madarakani sasa naomba kila halmashauri ipitie  ahadi alizozitoa wakati akiomba kura alipopita halmashauri zetu, fanyeni tathmini na andaeni ripoti inayoonyesha zilizotekelezwa, zinazoendelea kutekelezwa na zile ambazo bado kabisa, katika hilo ainisheni changamoto zake.

“Sote tunajua Mhe.Rais wetu anarudi kwa wananchi ifikapo 2020 kuomba ridhaa tena, hivyo ikiwa atapata ripoti hizi itamsaidia kwa kipindi hiki kujua ahadi zilizobaki na kuzitekeleza, najua tunapozunguka sisi tumebaini moja ya changamoto iliyobaki kubwa ni upungufu wa madaktari na  walimu,”alisema.

Majaliwa ambaye katika hotuba yake ilikuwa imejikita kujibu maombi ya risala ya ALAT iliyosomwa na Mwenyekiti wake,Gulamhafeez Mukadam,alisema mwaka huu ni wa uchaguzi hivyo aliwaagiza wakurugenzi kuendelea kuratibu uchaguzi wa Serikali za mitaa  na kuhamasisha wananchi kujiandikisha.

“Endeleeni kuratibu shughuli zote za uchaguzi wa Serikali za mitaa hadi hapo tutakapotangaza vinginevyo, anzeni maadilizi kwani miongozo tumetoa, toeni fursa na haki kwa yeyote mwenye sifa, pia kumbukeni kuwa nimezindua uboreshaji wa daftari la wapiga kura , maboresho yanahusisha na uchaguzi mkuu  wa mwakani hivyo mwenye umri wa miaka 17 akajiandikishe maana mwaka kesho atakuwa na miaka 18.

“Katika risala yenu nimesikia maombi mengi sana lakini nianze na hilo la posho kwa madiwani, niseme Rais wetu Mhe. Magufuli ametusihi tuwe na subira kidogo, vivyo hivyo kwa ombi letu la kuinua mgongo kwani kuna timu inafanya tathmini ya suala  hilo na itakapomaliza kazi yake pengine tunaweza kupata matunda.

“Kuhusu mgawanyo wa vijiji, kata, wilaya na mikoa, niseme hili nalo Serikali imelisimamisha kidogo kwa sababu tulibaini kuwapo na utitiri wa halmashauri halafu hazina ofisi, wafanyakazi wanarundikana katika ofisi moja, ngoja tuendelee kutatua changamoto zilizopo kwanza ndio tuendelee kufikiria hilo, kikubwa tutaleta fedha za kumalizia majengo yote ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi ili yaweze kumaliziwa,”alisema.

Mhe.Majaliwa aliwataka wenyeviti wa halmashauri na wakurugenzi kusimamia miradi ya maendeleo huku akishangazwa na namna baadhi ya majiji nchini yalivyoshindwa kuanzisha miradi mikubwa ya maendeleo ya kuwaingizia kipato na badala yake wamebaki kulalamika Serikali kuu kuwanyang’anya vyanzo vya mapato.

Alisema Serikali haijafanya kosa kukusanya fedha yote katika mfuko mmoja kwani walifanya tathmini na kuona ni heri fedha ikatunzwa eneo moja na kufafanua kuwa tangu mfumo huo uanze kumekuwepo na miradi mikubwa inayogharimu zaidi Sh. bilioni tano lakini kabla ya hapo kulikuwa na miradi midogo midogo yenye thamani Sh.milioni 700 ingawa mapato yao ni makubwa.

“Tumeelekeza kila halmashauri kubuni mradi wa kimkakati na kutuletea kwa ajili ya kuwapa fedha lakini baadhi ya wakurugenzi wameshindwa kufanya hivyo, hawajui hata kuandika andiko, wakiandika wakileta linatupwa sasa kama hamjui kutetea kile unachokitaka kuanzisha  ni heri ukakodi mtu akuandikie.

“Mpaka sasa halmashahuri 17 zimekidhi matakwa katika miradi 22 hawa tunawapa mabilioni ya fedha ili kuanzisha miradi wa kimakakati, awamu ya pili  halmashauri 12 zimeonekena kukidhi vigezo nazo zitapewa lakini changamoto ninayoiona ni  kutokamilika kwa wakati kwa miradi, watu hawasimamii ipasavyo, wapo wazembe na wanafanya kazi kwa mazoea, jambo lingine ni kutofanya upembuzi yakinifu vizuri.

“Ndiyo maana inafikia hatua Mhe. Rais Magufuli anakuwa mkali kwenu hasa kwa wale wanaofuja fedha, naomba kila halmashauri ipange mipango ya maendeleo, pesa zile zinazokuja zikiwa na maelekezo ya  kufanya kazi yake bila kubadilishiwa matumizi, tunahitaji kuona kila kijiji kinakuwa na zahanati,”alisema.

Mhe.Majaliwa aliendelea kusema  mbali na kuzitaka  halmashauri 10 za mwisho ambazo zilitajwa  kwa kushindwa kukusanya mapato na kufikia asilimia 80 zijitathmini na kuona namna ya kutojirudia kitendo hicho katika makusanyo yao ya mwaka 2019/2020 mbapo aliunyoshea kidole Mkoa wa Kigoma ambao halmashauri zaidi ya mbili hazikufikia lengo.

Hata hivyo alisema kilichosababisha Mhe.Rais Magufuli  kushindwa kufika katika mkutano na kumwakilisha ni kutokana na kuwa na vikao vizito  na wageni kutoka ndani na nje ya nchi  vinavyohusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika nchini.

Pia Mhe. Majaliwa alidokeza kuwa Serikali iliamua kumuondoa aliyekuwa katibu mkuu wa ALAT Taifa ambaye hakumtaja jina na kusema alikuwa anafanya mambo ya ovyo ya kuisemea Serikali na kuingia mikataba ya ovyo jambo ambalo lilikuwa halileti sura nzuri kwa Tanzania.

Alisema Serikali iliamua kumtafuta mbadala wake kwa kuzingatia sifa na kumpata Elirehema Kaaya ambaye anafaa kuiongoza ALAT na siyo huyo waliyemuondoa ambapo  aliyekuwa  ndani ya Tamisemi.

Awali, katika risala  Mwenyekiti wa ALAT, Mukadam, alisema moja ya changamoto kubwa inayowakabili ni posho  ndogo na kiinua mgongo cha madiwani ambapo aliomba Serikali kuongeza na kufikia asilimia 60 kwani kazi wanayofanya ni kubwa ya kuwahudumia wananchi na kuwatafutia kura wabunge na Mhe. Rais.

Pia aliomba kufanyika kwa mgawanyo wa kata, vijini na mitaa kwani baadhi ya maeneo ni makubwa sana jambo ambalo linaleta changamoto kwa viongozi hao katika kuwahudumia wananchi.



Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MWANZA, SIMIYU ZANG'ARA UTAMILIFU DARASA LA SABA KANDA YA ZIWA

    May 30, 2025
  • RAS MWANZA AZINDUA RASMI MRADI WA KUPAMBANA NA UGONJWA WA SELI MUNDU

    May 30, 2025
  • WAANDISHI WA HABARI MWANZA WAPIGWA MSASA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA WATOTO WA MITAANI

    May 29, 2025
  • RAS MWANZA AWATAKA VIONGOZI WA UMMA KUDUMISHA NIDHAMU NA UFANISI KAZINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.