• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Waziri Mkuu Majaliwa asisitiza Serikali kuendelea kushirikiana na Taasisi za kidini nchini

Posted on: October 17th, 2022


Serikali imesema itaendelea kushirikiana na taasisi za dini hasa zinazojikita kutoa huduma za jamii ikiwemo afya ili kuhakikisha watanzania wanakuwa na afya bora likiwemo Kanisa Katoliki.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 16, 2022 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati  akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando(BMC) baada ya kuzindua jengo la kutoa huduma  za macho hospitalini hapo  lililogharimu Sh bilioni 3.7 kati ya hizo ujenzi Shilingi bilioni 2.4 na vifaa bilioni 1.3.


Mhe. Majaliwa amesema uwepo wa hospitali ya BMC ambayo inatoa huduma za juu kabisa za kibingwa kama zinazotolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni faraja kwa wananchi wanaoishi Mikoa ya Kanda  ya Ziwa kwani Kanisa Katoliki limekuwa mstari wa mbele kutoa huduma katika sekta ya  Afya  pamoja na sekta zingine.


 Ameongeza kuwa, kwa miaka mingi Kanisa Katoliki limekuwa likijishughulisha na ustawi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake na kuhakikisha linamstawisha mwanadamu kiroho na kimwili linamiliki vituo vidogo vidogo vya kutolea huhuma za afya zikiwemo zahanati jumla 387.

"Idadi hiyo  inajumuisha hospitali za rufaa za ngazi ya mikoa ambazo zipo kwenye mikoa tisa, hospitali za wilaya 33 vituo vya afya 103 na zahanati 223 hakika mkakati huu wa kuendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kutujengea vituo karibu unafaa kupongezwa sana kwani mchango wa Kanisa Katoliki katika eneo la afya ni mkubwa sana,"ameeleza.

“Ninapozungumzia mchango wa Kanisa Katoliki katika eneo la afya ni mchango uliokithiri kwa serikali maana nalo linaendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutoa huduma za afya kwa wananchi wake, hospitali hii inatoa hudumza za kutosha kwenye maeneo yote,”amesema  Mhe. Majaliwa na kuongeza

 “Sasa imejiimarisha zaidi kwenye maeneo ya saratani na macho, hivyo wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa hawatalazimika kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 100 kwenda jijini Dar es Salaam kufuata huduma za saratani Ocean Road au kwenda CCBRT kufuata huduma za macho,”ameongeza  Mhe.Majaliwa.

Awali akimkaribisha Mhe. Majaliwa kuzungumza na wananchi waliofurika hospitalini hapo, Naibu Waziri wa Afya, Mhe.Dkt. Godwin Mollel amesema kukamilika kwa jengo hilo kutakuwa ni faraja kwa watu wenye matatizo ya macho kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kwani asilimia 4 ya watanzani wana matatizo ya macho na zaidi ya asilimia 90 ya matatizo hayo yanatibika.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya  Udhamini  ya BMC, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande  ameupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kufanya maboresho ya huduma za macho kwa haraka na kasi kubwa kwani zaidi ya miaka 40 tangu hospitali hiyo ianzishe walikuwa na daktari bingwa wa macho mmoja tu ambaye alikuwa anahudumia kanda nzima sasa  wapo madaktari bingwa sita wawili kati yao ni madaktari bingwa bobezi wa macho.

“Kukamilika kwa jengo hili pamoja na vifaa vya kisasa kunasababisha tuone changamoto ya upungufu wa rasilimali watu, hivyo tunaiagiza hospitali pamoja na Chuo Kikuu cha CUHAS waanze kufikiria namna ya kuanza kuzalisha wataalamu wa afya ya macho hapa hapa bugando maana wataalamu bingwa na bobezi wanao hapa hospitalini, vifaa tiba wanavyo, wagonjwa wapo, wahisani wapo na serikali nayo ipo kwa ajili ya kutoa miongozo na kutusaidia,”ameagiza Askofu Nkwande.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi akisoma taarifa ya siku ya macho duniani kwa Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa amesema Takwimu za Shirika la Afya Duniani zimeonyesha kuwepo kwa ongezeko kubwa la idadi ya watu wenye ulemavu wa kutokuona na upungufu wa kuona iwapo kusingechukuliwa jitihada mbalimbali kwani  zaidi ya asilimia 75 ya matatizo yote ya kutokuona yanayoikabili dunia yanachangiwa na sababu zinazoweza kuzuilika ama kutibika kwa gharama nafuu.

“Kwa kutambua hilo Tanzania inaandaa na kutekeleza mpango mkakati wa afya ya macho kwa vipindi tofauti, aidha sekta ya afya imeendelea kuimarisha rasilimali watu, miundombinu, vifaa na vifaa tiba kwa utolewaji wa huduma za macho ikilinganishwa na mwaka 2003 tulipoanza mkakati wa dira ya mwaka 2020 na uzinduzi wa jengo hili leo ni mchango wa serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata afya ya macho,”amesema Profesa Makubi.


Mkurugenzi wa BMC Dkt. Fabian Massaga amesema jengo hilo ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100 linakidhi viwango vya kimataifa na kitaifa kwani linauwezo wa kutoa huduma za kliniki, vipimo, huduma ya miwani, chumba cha upasuaji, wodi zenye vitanda 50, ukumbi wa mikutano na ofisi za wafanyakazi huku akibainisha kwamba vifaa vyote vya tiba na samani za ofisi zimekwishanunuliwa.


“Ujenzi wa jengo hili ulianza rasmi Machi, 2, 2021ulikamilika Juni 12, 2022 kliniki hii imeanza kutoa huduma rasmi Agosti 15, 2022 hadi sasa kuna ongezeko kubwa la wagonjwa ukilinganisha na kliniki ya awali ambapo wastani wa wagonjwa ilikuwa ni 70 kwa siku sasa ni wastani wa wagonjwa 120 kwa siku ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 42 ndani ya miezi miwili,”amesema Dkt. Massaga.


Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amefafanua kwamba mkoa huo una jumla ya vituo 457 vya kutolea huduma za afya kati ya hivyo 29 vinamilikiwa na taasisi mbalimbali za dini na kwamba matamanio ya mkoa huo ni kuwa kitovu katika kutoa huduma za afya za kibingwa ambapo ametoa wito kwa taasisi nyingine za dini kuwekeza katika sekta ya afya.


BMC inamilikiwa kwa ubia na serikali pamoja na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC).

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.