• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Zaidi ya Wananchi Elfu 72 kunufaika na Mradi wa Kituo cha Afya Budushi-Kwimba

Posted on: August 3rd, 2023

Zaidi ya Wananchi Elfu 72 kunufaika na Mradi wa Kituo cha Afya Budushi-Kwimba


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala bora, Mhe. George Simbachawene ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Mwanza kusimamia kwa nguvu zote utekelezaji wa miradi ya zaidi ya Bilioni 100.5 inayotekelezwa na Mpango wa TASAF kwenye Mkoa huo ili iwe bora na ikamilike kwa wakati.

Mhe. Simbachawene ametoa agizo hilo leo tarehe 03 Agosti, 2023 wakati akikagua ujenzi wa majengo ya jengo la Maabara, Wodi ya Wazazi na Upasuaji yanayotekelezwa kwa zaidi ya Milioni 291.8 zilizotolewa na Serikali kuu chini ya mpango wa TASAF huku zikitarajiwa kuwanufaisha zaidi ya wananchi Elfu 72 kutoka kwenye kata tano.

"Lengo la miradi ya TASAF ni kupambana na umasikini na kuboresha maisha ya watanzania, moja kati ya maeneo yanayonyong'onyeza ni mwananchi kukosa matibabu anapougua ila sasa hapa Serikali imeonesha nia ya kuboresha maisha ya mtanzania" Mhe. Simbachawene.

Mhe. Waziri amefafanua kuwa kila mmoja ana wajibu wa kusimamia ujenzi na utekelezaji wa miradi ya TASAF kama miradi mingine inavyofanywa kwani fedha hizo zinatolewa mahsusi kuwahudumia wananchi kuwaondoa kwenye adha mbalimbali kama Miundombinu ya barabara, afya, elimu na mingine.

"Hongereni kwa kujenga kituo kizuri cha afya, suala la kupata gari la wagonjwa kwenye kituo hiki haliepukiki hivyo niwaahidi tu kuwa nitalifanyia kazi ombi la Mhe. Diwani ili muweze kupata gari la wagonjwa kwenye kituo hiki." mefanua Mhe. Waziri wakati akijibu ombi la Diwani wa kata hiyo.

Aidha ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Kwimba kwa kuanzisha ujenzi wa kituo cha afya kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo ya zaidi ya Milioni 300 zilizopelekwa hapo kujenga jengo la wagonjwa wa nje, wodi za wanaume na wanawake pamoja na Miundombinu ya choo.

"Kwa ninavyofahamu uendashaji wa Halmashauri, ni lazima maamuzi haya yamewatia kwenye lawama sana maana watumishi wengi wanatamani fedha za mapato ya ndani zinaenda kutumika kwa kulipana posho ila nyie mliamua kuleta mradi huu wa muhimu wa wananchi." Amefafanua Simbachawene.

Vilevile, ametoa siku 30 kwa TASAF Makao Makuu kwa kushirikiana na TAKUKURU kufuatilia kwenye Mitandao ya simu ili kubaini kiasi na sababu ya upotevu wa fedha zilizohaulishwa kwa wananchi masikini kupitia mitandao ya simu na kusababisha kutowafikia walengwa na hatua kali zichukuliwe kwa wahusika.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija ametumia wasaa huo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwapatia zaidi ya Bilioni 1.5 kujenga Miundombinu ndani ya Wilaya hiyo chini ya mfuko wa huduma za jamii na amewapongeza wananchi kwa kuchangia nguvu kazi kwenye ujenzi.

"Miradi hii imekua na manufaa makubwa kutokana na kwamba inakwenda kuwagusa wananchi moja kwa moja na kwakweli tunampongeza Mhe. Rais kwa kutuletea fedha kupitia mradi wa kunusuru kaya masikini kwani ameonesha nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi kupitia huduma za jamii", Amefafanua Mhe. Mkuu wa Wilaya.

Naye Ndugu John Steven, Mkurugenzi wa Miradi kutoka TASAF Makao Makuu amefafanua kuwa pamoja na miradi mbalimbali ya ujenzi wa Miundombinu zaidi ya wanufaika Elfu 11 wanapata uhaulishaji wa fedha za kuwanufaisha kujikimu na kwamba kwa mkoa kuna wanufaika zaidi ya elfu 71.

Aidha, ametoa wito kwa viongozi kuhakikisha kamati za ujenzi za vijiji zinahusika moja kwa moja kwenye utekelezaji wa Miundombinu na akatoa wito kusimamia kwa karibu na kuongeza kasi ili ujenzi uweze kukamilishwa kwa wakati na huduma zianze kutolewa kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi.

Akiwasilisha taarifa ya Ujenzi wa Mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Emanuel Lameck ambaye ni Mtendaji wa Kata ya Sumve amefafanua kuwa majengo hayo Matatu kwa pamoja yanatekelezwa kwa zaidi ya Milioni 291 kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii chini ya mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.

Naye Mhe. Gelfasi Kitwaga, Diwani kata ya Sumve amewasilisha ombi kwa Mhe. Waziri la kupatiwa msaada wa Geri la kubeba wagonjwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi zaidi ya Eldu 72 wa Tarafa ya Ngulla.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.