IGP WAMBURA AFANYA MAZUNGUMZO LEO NA RC MTANDA
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura, leo Julai 19,2024 amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda wakati alipomtembelea ofisini kwake na kujadiliana masuala mbalimbali kuhusiana na hali ya usalama Mkoani humo.


