Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel leo Julai 4, 2022 ameendelea kuongoza zoezi la kuwapatia mahitaji muhimu na ukaguzi wa Ukarabati wa Vitanda na ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bwiru kufuatia kuunguliwa mwishoni mwa wiki.
Mhe Gabriel amewakabidhi Wanafunzi 76 Sabuni, Kalamu, Ndoo, Vikombe, Sahani na dawa za meno vyenye thamani ya Tshs Milioni 1.4 vilivyotolewa na Benki ya NBC tawi la Mwanza.
"Kwa niaba ya Mkoa tunashukuru benki ya NBC kwa msaada huu, walichofanya hapa ni kutimiza shauku ya wazazi kuona watoto wao wanaendelea na masomo na msaada huu tumeupokea na tunawashukuru sana kwa kutembea nasi kwenye vipindi vizuri na vipindi vigumu." Mkuu wa Mkoa.
Bwana Thomas Lijaji, Meneja wa NBC Mwanza amesemaa benki ya taifa ya biashara wamepokea kwa masikitiko taarifa ya kuunguliwa kwa moto kwa bweni na wameona wasaidie kutatua tatizo kwa kadiri walivyojaliwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.