Bima ya Afya yahitaji Elimu – Mongella
MKUU wa Mkoa wa Mwanza,John Mongella amewataka Wenyeviti wa Halmashauri na viongozi mbalimbali wa mkoa kuweka utaratibu wa wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhumi wa bima afya.
Hayo aliyasema jana kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichohudhuliwa a viongozi mbalimbali wa Serikali ,dini na wanasiasa, alisema ni vema kuhakikisha wananchi wanapatiwa elimu ili waweze kutambua umuhimu wa kutumia bima ya afya.
” Nasikitika kuona watu hawatambui muhimu wa kujiunga na bima ya afya kwani hurahisisha matibabu na gharama yake ni ndogo tofauti na mtu ambaye hatumii huduma hiyo,” alisema Mongella.
Mhe. Mongella ameongeza kuwa ili kuweza kupunguza vifo kwa wananchi ni vema kila kiongozi kuweka utaratibu wa kuelimisha jamii katika maeneo yao lengo ikiwa kupunguza na kumaliza tatizo hilo kwani watapata matibabu wakati wote.
“Ili tuweze kupunguza vifo vya watoto na wananchi kwa ujumla ni vema kuweka utaratibu wa kuwaelimisha wananchi kuhusu kutumia bima ya afya kwani inasaidai pindi ukiwa hauna hela na unaumwa au kuuguliwa,”alisema Mongella.
Aidha, ni dhambi kuto hamasisha wananchi kuhusu kutambua faida ya bima ya afya ambayo ni mkombozi kwa wenye hali ya chini kwani hutumia pesa nyingi katika matibabu wakati viongozi wanatumia na wamejiunga huduma hiyo.
Naye Clement Pancras Mwenyekiti wa ‘Chama cha Democratic Part’ (DP) alisema ni vema kwa viongozi kuhamasisha wananchi katika mambo ya msingi ikiwemo bima ya afya kwa ustawi wa maisha yao na taifa kwa ujumla.
Alisema kila mwanachi atakapokuwa na bima itasaidia hasa wenye hali ya chini ingawa changamoto iliyopo ni upatikanaji wa dawa ambao itamlazimu mgonjwa kutoa fedha za kununulia, hivyo aliiomba serikali kupeleka na kuhakikisha dawa zote zinapatikana katika hospitali zote na kuleta maana halisi ya kutumia huduma hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.