Serikali imesema sera iliyopo ya sekta ya kilimo inayotumika kwa sasa ndiyo cha chanzo cha wakulima kuwa masikini kutokana na kuwatumikisha wananchi kuilisha nchi na matajiri huku wakiwa wanakabiliwa na changamoto kubwa.
Kutokana na hali hiyo, imesema sera hiyo imepitwa na wakati ambapo wizara ya kilimo imelazimika kuanza kuipitia upya na kuondoa changamoto na vikwazo kwa wakulima ikiwa lengo ni kuihuisha sekta hiyo kutoka kilimo cha kujikimu na kuwa cha biashara kwa kuruhusu uwepo wa uwekezaji mkubwa.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akifungua sherehe za wakulima na maonyesho ya kilimo (Nanenane) katika viwanja vya Nyamhongolo mkoani Mwanza ambapo alipiga marufuku viongozi kuwazuia wakulima kuuza chakula chao kwa kuhofia uwepo wa njaa.
Bashe alisema kila mkulima anajua namna anavyotunza na kuilisha familia yake hivyo kama kuna kiongozi anahofia uwepo wa njaa ni vema akanunua mazao hayo kwa bei anayotaka mkulima na kuyatunza ili yaweze kusubiria dhana aliyoiweka kichwani kwake kwamba kutakuwapo na uhaba wa chakula.
“Hatuwezi kujenga viwanda wakati wakulima ni masikini wa kutupwa, ni lazima tuwawezeshe kwa kutengeneza mazingira ya watu kunufaika na kilimo chao sambamba na kuwa na soko la uhakika, ndio maana leo hii kama wizara tumeanza kupitia sera ya kilimo na kuondoa changamoto na vikwazo vilivyokwekwa .
“Sera iliyopo imepitwa na wakati kabisa, inawaumiza wakulima na kuwafanya kubaki kila mwaka kuilisha nchi na matajiri huku wao wakibaki na umasikini wao huku kukiwapo na utitiri wa taasisi nyingi ambazo ukichunguza zimeanzishwa kwa lengo la kuwakandamiza wakulima, hii haiwezekani kama wizara tumeanza kuangalia ni taasisi gani zinatkiwa kufutwa na kubaki chache .
“Fedha ambazo zilikuwa zikielekezwa kwenye utitiri wa taasisi hizo, zitaelekezwa katika mfuko maalum amboyo Wizara tunatarajia kuanzisha na kazi ya mfuko huo ni kufidia mkulima pale inapotokea mtikisiko wa bei katika soko la dunia, kama serikali hatuna uwezo wa kuthibiti bei ya soko la dunia lakini mfuko huo ndio utakaokuwa na kazi ya kutafuta pesa kwa ajili ya kuwafikia wakulima,”alisema.
Bashe alisema kama Serikali ilikuwa ikipokea fedha nyingi kutoka mataifa ya nje ili kuendeleza kilimo lakini zilikuwa zikiishia katika semina mafunzo kwa watendaji huku asilimia 50 ya fedha zilizokuwa zikipokelewa ndizo zinafika kwa wakulima, hivyo wizara imeanza uchunguzi wa matumizi hayo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.