• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA

Posted on: February 4th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesisitiza kuwa maendeleo ya zao la choroko yanahitaji mshikamano na ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, wakulima, sekta binafsi na wadau wa maendeleo.

Mhe. Mtanda amesema kupitia ushirikiano huo choroko linaweza kuwa zao la kimkakati lenye mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa na ustawi wa wananchi.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la choroko uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nyerere Gold Crest, Mhe. Mtanda amesema Serikali kupitia Taasisi na Mamlaka zake imeweka mfumo imara wa uzalishaji, ukusanyaji, uhifadhi, uuzaji na malipo ya mazao kwa kutumia stakabadhi za ghala na minada ya kidijitali ili kuhakikisha soko la uhakika na bei imara kwa wakulima.

Aidha, amewahimiza Wakuu wa Mikoa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sera, sheria na miongozo ya Serikali, kuhamasisha wakulima kujiunga na vyama vya ushirika, pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa uwekezaji katika uhifadhi, usindikaji na biashara ya choroko.

Kwa upande wa wakulima, Mkuu wa Mkoa amewahimiza kutumia mbegu bora na kufuata kanuni bora za kilimo, kuvuna kwa wakati, kuzingatia taratibu za ukaushaji na uhifadhi, kuuza kupitia mifumo rasmi ya masoko, na kushirikiana na maafisa ugani pamoja na vyama vya ushirika ili kutatua changamoto za uzalishaji na masoko.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Bi. Irene Mlola amesema ushirikiano wa wadau umeleta mafanikio makubwa ambapo Tanzania imeanza kutambulika kimataifa kama nchi inayothamini wakulima wake, kuwasajili katika mifumo rasmi na kuongeza tija kuanzia uzalishaji hadi sokoni.

Bi. Mlola amebainisha kuwa katika msimu wa mauzo ya choroko wa mwaka 2025, jumla ya tani milioni 23.4 ziliuzwa kupitia minada na mifumo rasmi, na kuingiza zaidi ya shilingi bilioni 28.9.

Ameongeza kuwa Mamlaka imeendelea kutoa miongozo, mafunzo kwa maafisa ugani na kuhamasisha uwekezaji, huku mikoa ya Simiyu, Mwanza na Shinyanga ikiongoza kwa uzalishaji na mauzo katika mfumo rasmi.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA

    February 04, 2026
  • KANDA YA ZIWA YAPIGWA MSASA UWEKEZAJI, DIRA YA TAIFA 2050 YATAJWA MSINGI WA MAPINDUZI YA UCHUMI

    February 04, 2026
  • RC MTANDA AWATAKA WAKANDARASI WA UMEME MWANZA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

    February 02, 2026
  • MADIWANI MWANZA WAJENGEWA UWEZO UONGOZI NA USIMAMIZI WA MAENDELEO

    February 02, 2026
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.