• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Hatimaye Shilima Yapata maji

Posted on: July 4th, 2019

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amekabidhi ujenzi wa mradi wa maji wa Shilima Wilayani Kwimba kwa Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA) baada ya Mkandarasi Kampuni ya Palemon Construction Ltd ya Mwanza kushindwa kukamilisha kwa wakati.

Makabidhiano hayo yalifanyika Julai 3, 2019 katika Kijiji cha Shilima na kushuhudiwa na watendaji mbalimbali wa Serikali na mamia ya wananchi wa Shilima na maeneo ya vijiji vya jirani.


Akizungumza kabla ya kukabidhi mradi, Waziri Mbarawa alieleza kwamba ujenzi wake ulianza tangu mwaka 2013 na kwamba ulipaswa kukamilika ndani ya miezi sita lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika.

Alisema Serikali iliamua kusitisha mkataba na Mkandarasi ambaye alishindwa kutekeleza ujenzi wa mradi kama ilivyo kwenye makubaliano.

Mara baada ya kuukabidhi mradi huo, Profesa Mbarawa aliiagiza MWAUWASA kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya Siku 60 ili kuwaondolea mateso ya muda mrefu wanachi wa maeneo hayo hasa ikizingatiwa kwamba mradi ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2013.

“Tunataka wataalam hawa wafanye kazi usiku na mchana na baada ya miezi miwili wananchi wapate maji safi na salama, uwezo tunao, tunaweza kumaliza tatizo la maji hapa kwa muda mfupi sana,” alisema Profesa Mbarawa.

Aliongeza kuwa kuna miradi ipatayo 88 kote nchini ambayo ujenzi wake ulianza kati ya Mwaka 2010 hadi 2015 ambayo ilipaswa kuwa imekwisha kamilika lakini hadi hivi sasa bado inasuasua na huku akiutolea mfano mradi huo wa Shilima.

Alibainisha kwamba Serikali kupitia Wizara ya Maji imeamua kuwa na utaratibu mpya wa kuzikabidhi Mamlaka za Maji miradi ambayo ujenzi wake una changamoto inayosababisha isikamilike kwa wakati.

“Tumeamua kubadilisha utendaji wa Sekta ya Maji, kila mahala tatizo ni maji, hili halikubaliki, tumejipanga na tunadhamira ya dhati kuhakikisha kero hii inakuwa historia kote nchini,” alisema Waziri Mbarawa.

Kuhusu utaratibu huo mpya, Profesa Mbarawa alibainisha kuwa ni wa nchi nzima na kwamba wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza miradi waliyokabidhiwa kwa wakati hawatovumiliwa na watanyanganywa na itakabidhiwa kwa Mamlaka za maji kwenye maeneo husika.

“Tumeamua miradi yote yenye changamoto tutaisimamia wenyewe na tutahakikisha inafanya kazi. Wananchi wamechoka kuendelea kuisubiri miradi hii ikamilke, fedha nyingi zinapotea, Serikali haitokubaliana na Mkandarasi anaechelewesha ujenzi wa mradi tayari tumefanya hivi Rungwe na sasa tumefanya hapa Shilima,” alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga alisema wamepokea agizo hilo la kutekeleza mradi huo ambao umesuasua kwa kipindi kirefu na kwamba wataukamilisha kwa wakati kama ilivyoagizwa.

“Tunaahidi hadi kufikia Septemba 3, 2019 tutakuwa tumeukamilisha mradi kwani itakuwa tayari ni Siku 60 na wananchi wataanza kupata majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria,” alisema Mhandisi Sanga.

Aidha, kwa mujibu wa Mhandisi wa Maji, Wakala wa Maji Vijijini Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Boaz Pius ni kwamba mradi huo utakapokamilika utahudumia wakazi 16,675 kutoka vijiji vinne ambavyo ni Shilima chenye wakazi 7,526, Mhande chenye wakazi 1,967, Kasang’wa wakazi 2,730 na Kijiji cha Izizimba “A” chenye wakazi wapatao 4,452.

Mhandisi Boas aliongeza kwamba kukamilika kwa mradi huo pia kutaweza kuhudumia vijiji vya Sangu, Gurumwa, Mwalubungwe na Kikubiji, ambapo bomba kuu linapita.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.