Hongereni Benki ya CRDB kwa ubunifu unaofanya mzidi kuwa taasisi bora: RAS Balandya
Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana ameipongeza Benki ya CRDB kwa ubunifu wake wa kibiashara unaofanya izidi kuwa taasisi bora na kuaminiwa na wateja wake.
Mtendaji huyo wa Mkoa amesema hayo leo Januari 17, 2024 kwenye tawi la Mwanza la Benki hiyo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi zawadi za vifaa vya kielektroniki mshindi wa kampeni ya Tisha na Tembocard tukakiwashe Afcon, Marion Albert amebainisha kampeni kama hizo mbali ya kuwanufaisha wateja wake lakini inazidi kujiimarisha pia kichumi.
"Hadi sasa mna wateja milioni 4 nchi nzima, hii ni hatua ya kujivunia inayofanya mzidi kuwa taasisi yenye nguvu na hatua hii ni matunda ya jitihada zenu mbalimbali kama hizi tunazo shuhudia leo," Balandya
Meneja wa CRDB kanda ya ziwa,Lusingi Sita amesema kampeni hiyo imewapata pia washindi 8 waliopata tiketi ya kwenda kushuhudia kombe la Mataifa ya Afrika Afcon huku wanne wakiwa tayari wametangulia mechi za makundi na wengine watakwenda hatua ya robo fainali,"Meneja kanda ya Ziwa.
"Mshindi huyo aliyejinyakulia zawadi hizi zenye gharama ya Shs milioni 9 ameibuka kutokana na kufanya miamala mingi ndani ya Benki yetu na bado shindano hili linaendelea,"Lusingi Sita
"Naishukuru CRDB leo kujipatia zawadi hizi,Jokofu la kisasa,Luninga inchi 75 na radio ambazo zimenisogeza mbele kimaisha,nitaendelea kuwa mteja bora wa Benki hii,"Marion Albert mshindi kutoka Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.